Monday, November 2


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Wanahabari wakichukua tukio.
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo.

Nape akijiandaa kujibu maswali ya wanahabari yaliyokuwa yameulizwa (hawapo pichani).
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema kipo kwenye mchakato wa kumtafuta mgombea wake wa Ubunge Jimbo la Handeni mkoani Tanga baada ya kutofanyika uchaguzi kufuatia kifo cha mgombea wake kwa tiketi ya chama hicho, Abadallah Kigoda.
Akizungumza na wanahabari leo kwenye ofisi za chama hicho zilizopo mtaa wa Lumumba jiijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema kuwa, wajumbe wa kamati ya CCM wapo kwenye mchakato huo na kesho mgombea atapatikana.
Alisema kamati hiyo imeshachuja waliojitokeza kuomba nafasi hiyo ambao walikuwa 11 na sasa wamebaki wawili ambao ni Hamis Hamad na Omar Kigoda hivyo kesho watakaa kikao cha kumpata mgombea mmoja.

0 comments:

-