Mkurugenzi wa Endless Fame, Wema
Sepetu akiwa amesimama mbele ya meza iliyokuwa imesheheni keki
alizokuwa amendaliwa katika sherehe ya kuadhimisha siku yake ya
kuzaliwa iliyofanyikia ndani ya Ukumbi wa Wema Sepetu Hall, uliyopo
ndani ya jengo jipya la Millenium Tower.
Meneja
wa Wema (kushoto), Martin Kadinda, akimsaidia kukata moja ya keki
zilizokuwa zimeandaliwa muda mfupi kabla ya kuanza kuwalisha ndungu
jamaa na marafiki zake.
MKURUGENZI wa Endless Fame Wema Sepetu, usiku wa kuamkia leo aliweza kufanya kufuru ya aina yake kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake iliyofanyikia ndani ya Ukumbi wa Wema Sepetu Hall, uliyopo ndani ya jengo jipya la Millenium Tower, Kijitonyama jijini Dar.
Katika Sherehe hiyo iliyohudhuliwa na ndugu jamaa na marafiki zake ilifana kwa kiasi kikumbwa, ambapo Wema alipewa zawadi mbalimbali huku akionyesha zawadi yake ya gari jipya aina ya Range Rover la mwaka huu.
Mbali na gari pia usiku huo meneja wake Martin Kadinda aliweza kuonyesha baadhi ya bidhaa zenye nembo za Wema Sepetu ambazo zitakuwa zikiuzwa kwenye duka lake lililopo Mwenge TRA.
0 comments:
Post a Comment