Monday, October 5


Ni hits baada ya hits mtu wangu… msanii wa muziki wa Bongo Flava Vanessa Mdee anaziandika headlines kwenye kurasa za burudani jumatatu hii, baada ya kuachia hit single yake ‘Nobody But Me’ aliomshirikisha rapper kutoka South Africa K.O, Vanessa Mdee amewatangazia mashabiki wake kupitia page yake ya Instagram ujio wa single yake mpya ‘Never Ever’ inayopatikana kwenye Album yake Money Mondays!
veemoney2
Single hiyo mpya ya Vanessa imetayarishwa na Producer Nahreel wa The Industry amabye ndiye aliehusika pia kwenye utayarishaji wa hit single iliyopita ya Vanessa ‘Nobody But Me’… nimefanikiwa pia kupata time ya kumuuliza Vee Money sababu za yeye kuchagua tena kufanya kazi na hit maker wa single ya ‘Game’, Nahreel ambapo Vanessa alisema…


>>> “Napenda sana kufanya kazi na Nahreel kwasababu he is the best, mimi na yeye ni kama Timbaland na Aaliyah tukiwa pamoja, tunavibe vizuri sana…”<<< Vanessa Mdee.
veemoney4
Japo Vanessa mwenyewe hajaweka wazi tarehe na siku atakayoachia single yake mpya ila kwenye kuzungumza nae staa huyo alisema…
>>>“Umm single yangu mpya itakuwa released mwanzo wa wiki ijayo, bado nasubiria detail moja ya mwisho ikamilike then nitawatangazia tarehe ya uzinduzi… ninachoweza kusema kwa sasa ni kwamba single hii ni another big song!”. <<< Vanessa Mdee.
veemoney3
Nyimbo za Vanessa licha ya kuwa nzuri huwa zinabeba stori tofauti, Siri ilikuwa na stori yake, Hawajui pia ilikuwa na stori nzuri sana na single ya Nobody But Me ilikuwa inahusiana na mapenzi… je single hii mpya itabeba stori gani safari hii? Vanessa Mdee alisema…
>>> ” Single yangu mpya safari hii inaelezea stori ya mapenzi, ‘Never Ever’ is a fairytale love song!” <<< Vanessa Mdee.
Kama wewe ni shabiki wa Vanessa Mdee ichukue hiyo mtu wangu, ‘Never Ever’ itakuwa hewani mwanzo wa wiki ijayo na kwa mujibu wa Vanessa hii itakuwa single nyingine kubwa kutoka kwake!

0 comments:

-