STAA wa Pop nchini Nigeria anayetamba na Wimbo wa Dodo, Davido, ameweka wazi msimamo wake wa kutotaka kuigiza filamu tena.
Hivi karibuni staa huyo aliweka historia
mpya ya kufanya vizuri kwenye moja ya filamu za Nigeria Nollywood
aliyoigiza yenye jina la John Zerebe ikiandaliwa na binamu yake, Ikey
Ojeogwu,
Davido amesema kuwa, John Zerebe itakuwa
ndiyo filamu yake ya kwanza na ya mwisho kwake kuigiza. Ameongeza kuwa
hana mpango wa kuigiza tena kama baadhi ya watu wanavyomuomba, maana
malengo yake si kuwa muigizaji.
Davido alisema hayo hivi karibuni wakati
akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni nchini Nigeria, akijibu swali
la mtangazaji lililomtaka Davido kuelezea kwa nini aliigiza na sasa
anaamua kuachana na uigizaji, Davido alisema ndugu zake ndiyo
waliomshawishi kucheza filamu hiyo, hivyo kwa sasa hatowasikiliza tena
ila anahitaji kufanya kazi yake ya muziki na kuendelea kuupaisha muziki
wake ili uwafikie mashabiki wake kote duniani.
“Hicho ni kitu ambacho sitofanya, sidhani kama nitacheza filamu tena tofauti na hii ya John Zerebe Part 2”, alisema Davido.
0 comments:
Post a Comment