Monday, August 3

Ni zawadi gani ya ndoa unaweza kumnunulia wakala namba moja wa wachezaji duniani?
‘Super agent’ Jorge Mendes, wakala wa Jose Mourinho, James Rodriguez, Nani, Falcao, Angel Di Maria, Cristiano Ronaldo, anatarajia kumuoa mchumba wake wa siku nyingi, Sandra Barbosa Ureno.
 
Cristiano Ronaldo, ambaye ni mteja mkuu wa Mendes, atakuwa ‘best man’ katika harusi hiyo, na taarifa kutoka Ureno zinasema mshambuliaji huyo wa
Madrid anatarajia kumpa zawadi ya kisiwa atakachomnunulia Ugiriki.

Habari za Ronaldo kumzawadia Mendes zilianza kuripotiwa na mtandao wa Noticia.

Kwa mujibu wa ripoti, Ronaldo anatarajia kutumia Pound Milioni 50 kwa ajili ya kununua kisiwa hicho.

Mendes sio jamaa ambae ana maisha ya kikawaida kabiisa, utajiri wake unakadiriwa kuwa zaidi ya Pond Milioni 100 hivi.

0 comments:

-