Friday, July 31

Mwanamuziki wa Nigeria, Iyanya.
Lagos, Nigeria MWIGIZAJI wa kike wa Ghana, Yvonne Nelson, amesema wiki kadhaa zilizopita katika mahojiano kwamba mwanamuziki wa Nigeria, Iyanya, ndiye mtu kwa kwanza ambaye aliuvunjavunja zaidi moyo wake kwa penzi kubwa ambalo alilolionyesha kwake.
Mwigizaji wa kike wa Ghana, Yvonne Nelson.
Hata hivyo, mwanamuziki huyo alipofanya mahojiano na kituo cha televisheni cha MTV, alisema japokuwa kweli alikuwa na uhusiano motomoto na Yvonne Nelson, lakini hakuwa mtu wa kwanza kumpagawisha kimapenzi.

"Tulipoanza uhusiano na Yvonne Nelson, sikuwa na furaha kwani kila mtu alikuwa anafikiri kwamba mimi nilikuwa ndiye shetani aliyempagawisha mwanamke huyo.
Watu wananizungumzia mimi hadi leo, lakini, mbona hawawazungumzii wanaume wengine ambao walimpagawisha kabla yangu?” aliuliza Iyanya. Aliongeza kwamba pamoja na penzi lao kukoma, bado ni marafiki wa kawaida.

0 comments:

-