SKYNER Ally ‘Skaina’
amekiri kukutana na changamoto ya kuombwa rushwa ya ngono na baadhi ya
wazalishaji wa filamu (producers), ili aweze kuonekana kwenye filamu
mbalimbali, jambo ambalo anakiri kumkatisha tamaa katika safari yake ya
kufika mbali kisanii.
Akibadilishana mawazo na mwandishi wetu
hivi karibuni, Skaina ambaye anaendesha maisha yake kupitia uigizaji,
alisema kutokana na malezi bora aliyoyapata kutoka kwenye familia na
misingi ya kidini, vinamfanya kuwa mwanamke mwenye kujiheshimu na kwamba
anaamini katika kipaji halisi na siyo kuhonga rushwa ya ngono.
“Nimewahi kukutana na changamoto ya
kuombwa rushwa ya ngono na baadhi ya watengenezaji wa filamu, lakini
hakuna hata mmoja aliyefanikiwa, nimelelewa katika familia imara sana,
hata misingi ya kidini imenifanya kuwa mwanamke mwenye kujiheshimu,
nitaendelea kubana. Kama ipo, ipo tu,” alisema Skaina.
RSS Feed
Twitter
August 08, 2015
Unknown
0 comments:
Post a Comment