Monday, August 10

2Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Wilbroad Slaa na mkewe Josephine Mushumbushi.
Mwandishi Wetu
IMEVUJA! Siri ya kitu kilicho kichwani mwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Wilbroad Slaa kuhusu mustakabali wake wa kisiasa umedaiwa upo kwa mkewe, Josephine Mushumbushi, Ijumaa Wikienda imevujishiwa.

Dr-Wilbroad-Slaa 
Dk. Wilbroad Slaa.
Chanzo cha kuaminika kilicho karibu na mwanasiasa huyo, kimeliambia gazeti hili kuwa mke wa kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania, anafahamu uamuzi uliochukuliwa na mumewe, isipokuwa kinachosubiriwa ni siku ya kutoboa kwa Watanzania.

“Dk. Slaa ameshachukua uamuzi wake na mtu pekee anayefahamu alichokifikia ni mkewe, kinachosubiriwa hapa ni siku tu ya kuwahabarisha Watanzania, lakini kama kuna mtu zaidi mwenye kujua kwa kina mwisho wa suala hili kwa sasa ni mkewe,” alisema mtoa habari huyo bila kutoa ufafanuzi zaidi.
Alipotafutwa Dk. Slaa ili aweze kuzungumzia suala hilo, simu yake haikupatikana. Jitihada zinaendelea.
Sakata la Dk. Slaa na chama chake lilijitokeza baada ya Chadema kumkaribisha waziri mkuu aliyejihuzulu, Edward Lowassa aliyejiunga na chama hicho na kuteuliwa kuwania urais kupitia muungano wa Ukawa.

0 comments:

-