Monday, August 17


Katika pitapita zangu mtandaoni nimekutana na hii list ya wachezaji warefu zaidi katika Ligi Kuu Uingereza na wafupi zaidi katika Ligi Kuu Uingereza, nimeona nikusogezee Top 5 ya  mastaa wa soka warefu zaidi Uingereza na Top 5 ya mastaa wafupi.
Top 5 ya Mastaa wa fupi
5. Santiago Cazorla González huyu ni kiungo wa kimataifa wa Hispania anayeichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza yumo katika hii list ya wachezaji wafupi ana urefu wa futi 5’6,
santi-cazorla_g_2496350k
4. Huyu ni kiungo mshambuliaji wa Italia anayeichezea klabu ya Sunderland ya Uingereza Emanuele Giaccherini kuna kipindi aliwahi kuingia katika headlines ya kung’atwa
na Luis Suarez katika michuano ya komne la dunia 2014 iliyofanyika Brazil, ana urefu wa futi 5’5.
Emanuele+Giaccherini+Swansea+City+v+Sunderland+g8Tv-_lyM1hl
3. Vurnon Anita kutokea katika klabu ya Newcastle United ya Uingereza amezaliwa Uholanzi ana urefu wa futi 5’6.
Vurnon+Anita+Newcastle+United+v+Fulham+Premier+D37DKpSDSZ1l
2.Aaron Lennon huyu ni muingereza anakipiga katika klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza ni mfupi laikini ana uwezo mkubwa wa kukimbia yaani spidi urefu wake ni futi 5’5.
1409562252241_wps_11_Aaron_Lennon_of_Tottenham
1. Nathan Dyer ni winga mshambuliaji wa klabu ya Swansea City ya Uingereza, raia wa Uingereza ana urefu wa futi 5’5.
article-2081247-0F51CEF000000578-174_634x487Top 5 ya Mastaa warefu
5.Per Mertesacker ni beki wa kati wa klabu ya Arsenal ya Uingereza, raia wa Ujerumani ana umri wa miaka 30 ana urefu wa futi 6’6 ni moja kati ya mabeki warefu Uingereza.
gun__1429524372_mertesacker_reading
4. Thibaut Courtois ni golikipa wa Chelsea ambae amewahi kucheza klabu ya Atletico Madrid ya Hispania kwa mkopo kabla ya kurudi katika klabu ya Chelsea, mzaliwa wa Ubelgiji ana urefu wa futi 6’6 1/2.
Thibaut+Courtois+UEFA+Champions+League+Final+GLEfLL-PJTbl
3. Peter Crouch ni miongoni mwa wachezaji wa kiingereza warefu zaidi kulingana na umbo lake sio mpenzi wa matumizi wa magari ya chini siku zote hupenda kutumia magari ya juu amewahi kucheza katika vilabu vya Liverpool, Tottenham Hotspurs na sasa Stoke City ya Uingereza ana urefu wa futi 6’7.
8-Crouch-Getty
2. Fraser Forster ni golikipa wa klabu ya Southampton ana urefu wa futi 6’7, kazaliwa March 17 1988 Hexham Uingereza
33676-zoom

1. Costel Pantilimon ni golikipa kutoka Romania na ndiye mchezaji mrefu kuliko wote Uingereza anaichezea klabu ya Sunderland, ana urefu wa futi 6’8.
PA_SOCCER-Man-City-211483_6982095

0 comments:

-