Thursday, August 27


Ziona Chana anaishi na wake zake wote katika jengo lenye vyumba 100. Wake zake hufanya zamu kulala naye. 
Hutumia jumla ya kuku  kutengeneza chakula cha usiku.
 
Yeye ni mkuu wa familia kubwa zaidi duniani - na anasema kuwa 'amebarikiwa' kuwa na wake 39.
 
Vile vile, Ziona Chana ana watoto 94, - wakwe 14 na wajukuu 33.
Wanaishi katika nyumba yenye vyumba 100, yenye ghorofa nne ambayo imejengwa katikati ya vilima vya kijiji cha Baktwang katika jimbo la Mizoram nchini India, ambapo wake zake hulala katika vyumba vikubwa vya pamoja.
Familia yote ya Ziona yenye watu 181
Jengo la Ziona lenye vyumba 100 ndio jengo kubwa kabisa lililojengwa kwa kokoto katika kijiji chenye vilima cha Baktawng

Bw. Chana aliliambia gazeti la the Sun: 'Leo ninajihisi kama mtoto maalumu wa Mungu. Amenipa watu wengi kuwatunza.
'Ninajiona kama mwanaume mwenye bahati kwa kuwa mume wa wanawake 39 na kiongozi wa familia kubwa kabisa duniani.'

Familia hiyo inaendeshwa kwa nidhamu ya kijeshi, ambapo mke mkubwa Zathiangi huwasemamia na kuwapanga wenzake kufanya kazi za nyumbani kama vile kufanya usafi, kufua na kuandaa chakula. 

Katika mlo mmoja wa jioni hutumia kuku 30, humenya lb 132 za viazi  na kupika kilo 220 za mchele.
Wakati huo huo, Bw. Chana pia ni kiongozi wa madhehebu ya dini inayowaruhusu wafuasi wake kuoa wake wengi anaowataka.
Wanawake wakubwa katika familia ya Chana wakiwa katika maandalizi ya kutengeneza chakula
Bwana Ziona Chana katika picha ya pamoja na wake zake 39 nyumbani kwao katika kijiji cha  Baktawang, Mizoram, India

Alioa wanawake kumi katika mwaka mmoja, wakati wa ushababi wake, na hulala katika jumba cha pekee yake chenye kitanda kikubwa huku wake zake wakilala katika vyumba vya pamoja. 

Wanawake vijana zaidi huwaweka jirani na chumba chake huku wale wakongwe wakilala vyumba vya mbali - na kuna mfumo wa mzunguko kwa wale wanaolala naye. 
 
Rinkmini, mmoja wa wake wa Bw. Chana, ambaye ana uamri wa miaka 35 anasema: 'Tunakuwa karibu naye kwa sababu ndiye mtu muhimu zaidi katika famiia. Ndiye mwanaume mzuri na mwenye mvuto kuliko wote kijijini. 
Mwanamke huyo anasema kuwa Bw. Chana alimuona akitembea kijijini asubuhi moja miaka 18 iliyopita, akamuandikia barua ya kutaka kumuoa.
Chumba cha pamoja: Jengo la ghorofa nne linavyonekana kwa ndani. Jengo hilo hujulikana kama Chhuanthar Run - Nyumba ya Kizazi Kipya

Mke wake mwingine, Huntharnghanki, alisema kuwa familia yote inaishi pamoja. Inaelezwa kuwa familia hiyo inaishi kwa mfumo wa 'kupendana na kuheshimiana'
Naye Bw Chana, ambaye madhehebu ya dini yake ina wafuasi 4,00, bado anaendelea kutafuta wake wapya.
'Ili kupanua dini yangu, niko tayari kwenda hata Marekani kwa ajili ya kuoa,' alisema.
Mtoto wake mmoja alisisitiza kuwa Bw Chana, ambaye babu yake alikuwa na wake wengi, huoa wanawake maskini wa kijijini hapo ili apate kuwatunza. 

0 comments:

-