Mwenyekiti
wa Taasisi ya kilimo (TASO), Engelbert Moyo (kushoto)akizungumza jambo,
pamoja na Meneja wa mawasiliano wa kampuni ya simu ya mkononi ya Tigo,
John Wanyancha.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi katika maonesho ya
kimataifa ya sikukuu ya wakulima yajulikanayo kama Nanenane
yatakayofanyika mkoani Lindi, Agosti Mosi mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar
es Salaam, Meneja wa mawasiliano wa kampuni ya simu ya mkononi ya Tigo
ambao pia ni wadhamini wa maonesho hayo, John Wanyancha amesema kuwa
sikukuu ya maonesho ya wakulima kutakuwa na huduma mbalimbali
zitakazokuwa zikifanyika zikiwemo za kilimo.
Amesema kuwa mbali na huduma
zitakazokuwa zikitolewa pia wananchi kutoka maeneo yanayozunguka Mkoa wa
Lindi kama vile Mtwara wataweza kunufaika na huduma zitakazokuwa
zikifanywa na Tigo ambazo zinajulikana kama Tigo Kilimo, hivyo wananchi
wajitokeze kwa wingi.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Kilimo
(TASO), Engelbert Moyo amesema kuwa katika maonesho hayo wakulima
wategemee kuona teknolijia mpya kama vile mbegu za kisasa pamoja na
pembejeo hivyo maonesho hayo yataweza kuwavutia wawekezaji katika
nyanja mbalimbali kama vile; utalii, madini, mawasiliano pamoja na
nyinginezo.
Maonesho hayo ni ya 22 tangu kuanzishwa
kwake na yanatarajiwa kuhitimishwa Agosti 8, mwaka huu na Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.
NA DENIS MTIMA/GPL
0 comments:
Post a Comment