Monday, July 27


Bobbi Kristina Brown ,mtoto wa marehemu Whitney Houston ambaye alikuwa gwiji wa muziki wa R&B ,amefariki dunia baada ya kupoteza fahamu kwa muda wa miezi sita tangu alipokutwa taabani kwenye bafu lake na pindi alipofikishwa hospitalini na kukutwa na matatizo kwenye ubongo.
 
Bobbi amekufa akiwa na umri wa miaka 22,huku akivutiwa kuwa muigizaji na muimbaji mahiri na mwenye ubora wa aina yake.
 
Msemaji wa familia Kristen Foster amesema Bobbi amefariki akiwa amezungukwa na familia yake ,”hatimaye yuko salama sasa kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu.
 
Hata hivyo  amewashukuru wote walioungana nao katika maombi na kuonesha upendo kwa miezi michache iliyopita.

0 comments:

-