Thursday, June 4



Umewahi kusikia habari za Kadra Mohamed? kama bado ni lazima usikie.

Yeye ni mwanamke wa kwanza wa Somalia kuwa Afisa wa Polisi katika mji wa Minnesota nchini Marekani kuvaa hijabu akiwa kazini.


Kadra mwenye umri wa miaka 22 ameandika historia katika dunia.
Kadra amemaliza masomo ya mafunzo ya Upolisi mwezi Mei mwaka huu katika chuo cha St Paul Police Academy.
Alijiunga na St Paul mwezi Machi mwaka jana katika ulinzi shirikishi baada ya idara hiyo ya Polisi kupitisha sheria ya kuruhusu wanawake kuvaa Hijabu.


St. Paul ni moja ya idara chache za polisi nchini Marekani ambayo inaruhusu wanawake kuvaa Hijabu wakiwa kazini. Kwa njia hii wanamatumaini kuwawezesha wanawake wa kiislamu kutekeleza kazi zao vizuri na kuzingatia sheria.

Kadra alizaliwa katika kambi ya wakimbizi nchini Kenya mwaka 1991 baada ya wazazi wake kukimbia kutoka mji wa Mogadishu, nchini Somalia kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mama yake anaitwa Zamzam mwenye asili ya Somalia na baba yake ni mtu mwenye asili ya Ethiopia anaitwa hassan.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEioURyI5xF_BJl9F_1N7Zur53qkNajO3FaZOqj1glbiKyaAT7liMy86u2cnyAjG_KHHSv1yxpY6oHivZn-QMpkXK5AbPpwKRBKmoJj0jGHT2OT6F1fsBAGYzZknZGw0cJjheHh8jdm6ZFJ9/s400/kadra+polisi13.JPG
Kadra anatoka katika familia ya watoto wanne, wawili wa kiume na wawili wa kike, baba yake alifariki yeye akiwa na umri wa miaka 12.
Kuna wanawake mamilioni kama Kadra wanataka kufikia malengo yao lakini wanakwamishwa na sheria zenye kuwabana kutimiza wajibu wa dini yao.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4PsiJFBdgxBe6XOB7zqJc91ZhnB363E1XEAWz0FW5OuAXLQsE50Fwtb6BtokY1EEBG2EGvbPxfXByQWhDprmKZ91YPDSKCMDHstqu3x2zzZLh4trzH1TV2cD3KdYWkTqMZeqLZTOkgBDo/s400/hijab-police-woman.jpg
Ni muda sasa wa kuanza kushinikiza kuondolewa sheria zinazozuia waislamu kutokutimiza wajibu wa dini yao wanapokuwa makazini hususani polisi wanawake nchini Tanzania.

0 comments:

-