Thursday, June 4

kelly
Ongezeko la wadada wanaopenda au wanaotamani kuongeza makalio limekua likikua kwa kasi sana sehemu mbalimbali duniani huku wengi wakiamini ni fasheni.
Tunashuhudia watu wengi wakiongeza makalio kwa kusudi la kuwa wenye mvuto zaidi, na kumekuwepo na vidonge na sasa kuna sindano za kuongeza makalio.
Leo nimekutana na stori iliyotokea Los Angeles Marekani, ambako msichana Kelly Mayhew mwenye miaka 34 amefariki dunia baada ya kufikishwa katika Hosipitali ya St.John’s Espiscopal Hospital ikiwa ni muda mchache baada ya kuchomwa sindano ya kuongeza makalio.

Kelly Mayhew  Photo via Facebook
 Kelly Mayhew na mama yake walisafiri kutoka Maryland kwenda Rockaway,walikokua wameelekezwa na rafiki yake Kelly ili kwenda kuchoma sindano hiyo amabayo ilikua inatolewa kinyume kidogo na utaratibu na mtu ambaye alijiita daktari lakini hakua amesajiliwa na hatambuliki kisheria kutoa huduma hiyo.
Baada ya kuchomwa sindano hiyo Kelly alianza kupata shida kupumua na kujitupa ovyo chini akionekana kuishiwa pumzi na baada ya kuhangaika kwa muda usiopungua dakika ishirini Kelly alidondokea mikononi mwa mama yake na kukata roho.

0 comments:

-