Friday, May 1

Duniani kuna wanyama ambao wana sura mbaya sana, na hii ni top 5 list ya wanyama hao wenye sura mbaya.
wa kwanza ni


huyu anaitwa Daubentonia madagascariensis anapatikana katika kisiwa cha Madagascar ambaye ana mchanganyiko wa meno kama ya panya na kidole chembamba cha kati ili kukamilisha uwepo wake kimazingira kama gogota. Ni aina kubwa ya nyani duniani kati ya wanyama wanaotembea usiku mwenye sifa ya  kipekee ya kupata chakula kwa kuchimba miti ama kuingiza vidole vyake katika matundu yaliyoko kwenye miti na kutafuna. Ana uzito wa kilo 2.5, na majike wana uzito pungufu kidogo (kwa wastani wa gramu 100) ukilinganisha na madume. Mbali na uzito na viungo vya jinsia macho yao hayadhihirishi jinsia. Wote hukua kutoka cm 30-37 kutoka kichwa na mwili, na mkia 44-53 cm.

wa pili ni


huyu anaitwa Sphynx Cat Canada asiye na manyoya ni aina nadra sana ya paka na mwenye manyoya kidogo saaana, kwa maana nyingine manyoya mafupi saana juu ya mwili wake. Ngozi yao ni kama rangi ya manyoya yao, na paka wote kawaida huashiria mwelekeo (imara, uhakika, kasi, n.k). Wakati mwingine hufananishwa kimakosa na Chihuahuas kwa sababu ya muonekana wao ufananao na paka. Wao wana akili sana, wenye kujiamini na wapole, mara nyingi hupenda kukumbatia wamiliki wao, binadamu wengine, na wenyewe kwa wenyewe.


wa tatu ni

huyu anaitwa Babirusa au nguruwe-deer ni mnyama mwenye muonekano kama wa nguruwe anaepatikana maeneo ya Sulawesi na visiwa jirani vya Indonesia. Kwa kawaida Babirusa huwekwa kwenye kundi la aina moja ya Babyrousa, lakini utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kwamba kuna aina kadhaa zinazoweza kutofauitshwa kwa msingi wa jiografia, ukubwa wa mwili, kiasi cha nywele mwilini, na sura ya meno ya juu kwa madume.

wa nne ni

huyu anaitwa Viperfish (aina ya Chauliodus) ni samaki wa kina kirefu cha maji mwenye meno marefu kama sindano yanayochomoza toka taya ya chini. Hukua kwa urefu wa sentimita 30 hadi 60 (14 inches). Jina Viperfish pia wakati mwingine kutumiwa na weever mdogo

wa tano ni

huyu anaitwa Anglerfish, historia yake bado sijaijua sawasawa ila nawaahidi kuwa nafuatilia historia yake na mara nitakapoipata nitawawekea.

0 comments:

-