Stori
ambayo imechukua Headlines tangu asubuhi ya leo April 02 ni taarifa
kutoka kwa wenzetu Kenya kutokana na lile shambulio la kigaidi
limehusishwa na kikundi cha Kigaidi cha Al-Shabaab na hii ni baada ya kuvamia Garissa College University, huu ni muendelezo wa kile kilichoripotiwa mwanzo.
Mpaka sasa ripoti inasema Wanafunzi 70,
wameuawa na wengine zaidi ya 79, wamejeruhiwa kutokana na tukio la
uvamizi wa Garissa College University, wanafunzi walionusurika wamesema
magaidi hao walianza kuwapiga risasi walinzi wawili waliokuwa getini na
kuelekea katika mabweni ya wanafunzi ambapo walianza kuwagawa kwa dini
zao na kuanza kuwaua kwa risasi.
Kufuatia tukio hilo Rais Uhuru Kenyatta, amemtaka Inspector Generali wa Polisi, Joseph Boinet kuhakikisha wanamgambo wote wanaripoti kwenye chuo cha mafunzo ili kuongeza idadi ya maafisa wa Polisi nchini humo.
Amesema taifa hilo linakubwa na uhaba wa
maafisa wa Polisi kutokaza na kufutwa kwa zoezi la kuwasajili maafisa
wa Polisi, Serikali ya Kenya imetangaza kumzawadia shilingi milioni
ishirini za Kenya mtu yoyote atakaefanikisha kukamatwa kwa mshukiwa mkuu
wa shambulio hilo anaefahamika kama Mohhamed Mahamoud, Polisi bado wanaendelea na zoezi la uokoaji.
0 comments:
Post a Comment