Saturday, April 18

Sindano 
Zamani kulikuwa na misemo ambayo ilikuwa ikitumiwa sana, utasikia kazi f’lani ni wito.. ilikuwa kawaida yani, ukikutana na Mwalimu utaambiwa ualimu ni wito.. Daktari nae utasikia udaktari ni wito.. siku hizi sio maneno ambayo yanasikika sana.
unit
Nimekusogezea hii story toka Jamhuri ya Czech, muuguzi mmoja kafikishwa Mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha maisha.. kesi iliyofanywa ashitakiwe imenishtua kiukweli.

Unajua ikitokea mtu unaumwa au haujisikii vizuri unaenda zako Hospitali ili kucheki kama una tatizo ili utibiwe.. lakini kitendo cha huyu muuguzi kinaweza kukushtua na wewe pia, yeye kaamua kuyakatisha maisha ya wagonjwa, kisa alikuwa ameelemewa na kazi kwa hiyo akaona azidishe potassium kwa wagonjwa ili kupunguza mzigo wa kazi.
Vera Maresova ambaye umri wake ni miaka 50 aliyekuwa akifanya kazi katika hospitali moja iliyoko Rumburk ambapo amefanya kazi kwa miaka minne aliamua kuwachoma sindano zenye Potassium wagonjwa ambao ni wanawake watano na mwanaume mmoja kwa lengo la kuwaua.
Yani eti wagonjwa wanaohitaji huduma yake walikuwa wengi, akaamua kuwapunguza ili wabaki wachache aweze kuwahudumia.
Ripoti ya Uchunguzi wa Polisi inaonesha Maresova aliwachoma sindano zenye sumu hiyo wagonjwa hao kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 2010 na 2014, kesi imeisha na kahukumiwa kifungo cha maisha jela.

0 comments:

-