Thursday, February 19

obassss
Ukiwa kiongozi kwenye nafasi yoyote lawama huwezi kuzikwepa, tumesikia wananchi wakilalamikia matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa na viongozi, hizi lawama haziko bongo peke yake kuna hii kwenye headlines za India.
Waziri mkuu wa India Narendra Modi kununua suti ya gharama ambayo aliivaa kwenye mapokezi ya Rais Barack Obama alipotembelea India mwezi January nayo imekuwa ishu! headlines za vyombo vya habari India zimeandika kuhusu wananchi kulalamika gharama za suti hiyo, eti wanadai gharama haziendani na maisha ya wananchi wanavyoishi.

india
Waziri mkuu wa India, Narendra Modi akiwa na Rais Obama wa Marekani
Suti ya Waziri huyo iligharimu zaidi ya dola 16,000 (kama milioni 30 za kibongo), wananchi wanadai ametumia pesa nyingi kushona suti huku akishindwa kutekeleza ahadi ya kuboresha maisha yao.
Moja ya kitu kinachoifanya suti hii kuwa na gharama kubwa ni upekee wake, ina mistari midogo midogo ambayo ukiiangalia kwa ukaribu ni maandishi yaliyoandikwa jina la Waziri Mkuu huyo.
image (2)
Narendra Modi, Waziri huyo Mkuu akiwa kwenye suti hiyo.
Waziri Mkuu Ghandi ametangaza kuipiga mnada suti hiyo ili iuzwe na pesa itakayopatikana ichangie masuala mengine ya maendeleo kwa watu.
Makamu wa Rais wa India Rahul Ghandi naye ni kama anaunga mkono kinachosemwa na wananchi hao.

0 comments:

-