Wananchi
wakishuhudia janga la moto uliozuka mara baada ya transfoma la kituo
kikuu cha umeme Mgololo, Iringa kulipuka ghafla na kuteketea.
Moto ukizidi kuteketeza transfoma hilo.TRANSFOMA la kituo kikuu cha umeme eneo la Mgololo jirani na kiwanda cha karatasi mkoani Iringa limeteketea kwa moto baada ya kulipuka ghafla leo.
Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na umewaka kwa takribani saa nne kutokana na ukosefu wa zimamoto hali iliyopelekea kuitwa vikosi vya zimamoto kutoka Njombe na Mafinga kilomita 130 kutoka eneo la tukio.
Baadhi ya maeneo ya mikoa ya Njombe na Mbeya itakuwa gizani kwa kuwa yanatgemea umeme wa kituo hicho.
0 comments:
Post a Comment