AMA
kweli shetani anafanya hesabu zake za mwisho! Tangu mwaka 2014 uanze
yapo yaliyotokea na kusisimua likiwemo la kunaswa kwa kinara wa utoaji
mimba, Dk. Mambo, maeneo ya Kawe, Dar lakini hili la warembo kufumwa
wakitoa dozi ya ngono linaweka historia nyingine,
Hebu
sikia, saluni inayojihusisha na vitendo vya ’masaji’ lakini kumbe ngono
imo ndani yake imenaswa na kufumuliwa baada ya kukutwa uchafu wa aina
yake nyuma ya pazia.SOMA ZAIDI
Saluni
hiyo maarufu kuliko Miji ya Sodoma na Gomora, ipo maeneo ya Sinza
ambapo kwa muda mrefu sasa imekuwa ikijihusisha na uchafu huo na
kusababisha kero kwa wananchi wenye maadili yaliyotukuka.TAARIFA MEZANI
Oparesheni
Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, ikiwa imetulia ndani ya
mjengo wa makao yake makuu, Bamaga-Mwenge jijini Dar, Mkuu wa kikosi
maalumu cha Mtambo wa Kurekebisha Tabia (MKT) ambacho ni kitengo ndani
ya OFM, alipokea simu kutoka kwa msamaria mwema akitoa ‘tipu’ juu ya
ishu hiyo.
Mtoa
taarifa huyo alieleza malalamiko yake juu ya kero wanayoipata raia
waishio jirani na saluni hiyo kufuatia huduma chafu za kuchukiza ambazo
hufurahiwa na shetani na malaika wake tu.
Msamaria Mwema: Halooo.... halooo... jamani halooooo, hapo ni Makao Makuu ya OFM?
OFM: Ndiyo mama, tukusaidie nini?
Msamaria Mwema: Mna habari jamani?
OFM: Zimejaa tele, ila hata ya kwako inaweza kuwa bora kuliko tulizonazo.
Msamaria
Mwema: Hapa Sinza Kwaremi (Dar) kuna saluni moja inaendesha vitendo
vichafu vya ngono na hakuna sheria yoyote inayochukuliwa dhidi ya
wahusika.
OFM: Saluni ya ngono? Kivipi mama? Hebu fafanua tafadhali!
Msamaria Mwema: (kwa sauti ya juu mno) ninyi njooni mtajua kila kitu hukuhuku lakini inaendesha mambo ya ajabu (simu ikakatika).
OFM MZIGONI
Bila
kupoteza sekunde, mkuu huyo wa MKT, aliwapanga ‘makamanda’ maalumu na
kuwapa maelekezo muhimu ya jinsi ya kujua ukweli juu ya uovu uliodaiwa
kutendwa kwenye saluni hiyo.
UCHUNGUZI
OFM
iliwatuma vijana wake ‘watanashati’ hadi eneo lililotajwa ili
wachunguze kama kweli kuna saluni yenye jina lililotajwa na mtoa habari
wetu.
Baada
ya maelekezo hayo, vijana hao wakiongozwa na roho safi ya kunyoosha
maadili katika jamii, walifika hadi Sinza na kukuta saluni yenye jina
hilo ambapo walianza kufanya upelelezi wa hali ya juu mno huku wakiwa
makini kuliko hata neno lenyewe.
UTHIBITISHO
Baada
ya kutinga eneo hilo, OFM iliendesha upelelezi maalumu kwa kuwauliza
baadhi ya wakazi na watu wanaofanyia shughuli zao za kujiingizia riziki
na kupata ukweli halisi juu ya ufuska ufanywao ndani ya saluni hiyo.
Katika uchunguzi huo, OFM ilipata uthibitisho kuwa kweli ibilisi yuko katika hesabu zake za mwaka kwa kufanya uchafu wa kufuru.
Ilielezwa
kwamba, watumishi wa saluni hiyo ambao ni warembo, hujifanya wanatoa
huduma ya kuchua mwili (body massage) kwa Sh. 25,000/= kwa vyumba na
huduma za kawaida, lakini kwa vyumba vyenye choo na bafu kwa ndani (self
contained) ni Sh. 35,000/=.
HUDUMA
Katika
upelelezi huo, ilibainika kuwa mteja akilipia gharama ya vyumba vya
self contained, ana uhuru wa kuchagua kama atapenda kufanyiwa huduma ya
uchuaji kwa mikono tu au kwa matiti na wakati mwingine mwili mzima huku
mtoa huduma hiyo akiwa amevua nguo zote!
Ikazidi
kuelezwa kuwa, endapo mhudumiwaji atataka huduma hiyo ya mchuaji kuvua
nguo zote, atafanyiwa hivyo lakini kama atazidiwa na kuhitaji huduma ya
ngono, atatakiwa kuongeza Sh. 50,000/= kwa msichana huyo wa huduma na
kufanya gharama kuwa zaidi ya Sh. 80,000/=.
“Wamekuwa
wakifanya vitendo viovu sana, yaani ngono njenje, jamani hii siyo
saluni, bali ni danguro la ngono fuatilieni mtangundua juu ya ukweli
huu,” alisema mmoja wa raia katika upelelezi wa OFM.
OFM NDANI YA NYUMBA
Ili
kujiridhisha na maelezo hayo, timu ya OFM ilituma vijana wake tofauti
kwa muda wa siku tatu mfululizo na kubaini kuwa yote yaliyosemwa na
kutajwa kwa kirefu yanatendeka ndani ya saluni hiyo!
‘Askari’
wa kwanza wa OFM aliingia ndani ya saluni hiyo (jina linavunda kwenye
droo za meza yetu) na kuwakuta wahudumu wamejaa tele na alipowauliza juu
ya huduma ya masaji na ngono, walijibu kwa sauti ya furaha na bashasha
kubwa bila kujua kuwa kijana wetu alikuwa na vifaa maalumu vya kunasia
sauti.
“Ni
wewe tu jamani, kwani wewe ni mgeni maeneo haya? Mbona utaratibu
unaeleweka, lakini maelezo ni hayo kwa hiyo karibu sana,” alisema mmoja
wa warembo hao huku akilegeza macho mithili ya mgonjwa wa degedege.
Siku mbili zilizofuata, askari wa OFM waliendelea kupata stori na maelezo ya aina hiyohiyo.
MTEGO!
Siku
ya tukio, (mwanzoni mwa wiki hii) OFM iliweka mtego kwa kumpeleka
kijana wake ili ajifanye anahitaji huduma hiyo ya kufanyiwa masaji mwili
mzima na baadaye ajifanye amezidiwa na kuhitaji huduma ya ngono.
Katika
mtego huo, OFM ilitoa taarifa polisi ambapo ‘vijana wa IGP Ernest
Mangu’ hawakulaza damu, wakatoa ushirikino wa kutosha kwa OFM.
MTEGO WAFYATUKA
Kama
kawaida, OFM huwa haishindwi linapokuja suala la oparesheni maalumu
kama hiyo, fuatilia sana. Mtego wake ulifyatuka ambapo mmoja wa vijana
wake alijifanya kuhudumiwa (angalia picha ukurasa wa mbele).
Baada
ya kuweka mazingira sawa, OFM na polisi wa kike na kiume walivamia na
kufanikiwa kufuma laivu matukio mengi ya ufuska mkubwa (ukitaka kuona
zaidi, unakaribishwa Bamaga ofisini kwetu).
WAUME ZA WATU!
Baada
ya zoezi hilo kukamilika, baadhi ya mashuhuda (hasa akina mama)
walisikika wakishukuru kufumuliwa kwa saluni hiyo kwa kuwa ndoa zao
zilikuwa zimeanza kuota magugu kwani wateja wengi wa saluni hiyo ni
waume za watu na vigogo serikalini!
“Jamani
tunashukuru sana, waume zetu walikuwa wanakimbilia hapo, ugomvi kidogo
tu, mwanaume anakwenda hapo na akirudi nyumbani hana habari kabisa na
mkewe, safi sana OFM na polisi kwa jumla,” alisikika mama Joyce
akishangilia kufumuliwa kwa saluni hiyo.
SOO POLISI
Baada ya ‘sheshe’ hilo, warembo sita walikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi kwa upelelezi maalumu.
MMILIKI
Katika
upelezi wa awali, watumishi hao walimtaja mmiliki wa saluni hiyo kwa
jina moja la Chifu huku wakishindwa kuweka wazi na kufafanua kwa undani
zaidi.
KAMANDA WAMBURA UPO?
Gazeti
hili lilifanya jitihada za hali ya juu kumpata Kamanda wa Mkoa wa
Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura ili azungumzie juu ya sakata
hilo, lakini hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, simu yake ya
kiganjani ilikuwa ikiita bila kupokelewa
0 comments:
Post a Comment