Saturday, January 31



Huku kwetu tuna utaratibu wa kuwapa watoto wetu majina tunayopenda, yapo majina ya watu maarufu kama viongozi, wanasoka, waigizaji na wengineo.
Kuna hizi nchi ambacho wao wamepiga marufuku baadhi ya majina kupewa watoto, list ni hii hapa.
New Zealand: Msajili wa Vizazi, Vifo na Ndoa nchi hii ameagiza baadhi ya majina kupigwa marufuku ikiwemo majina haya;Majesty, Queen Victoria, Lucifer na jina laMafia No Fear.
VenezuelaWao wamezuia matumizi ya jina la Superman kwa kuwa ni gumu kulitamka.
Denmark: Wametoa list ya majina rasmi ambayo yako zaidi ya 7,000 mtoto akizaliwa anachaguliwa jina kati ya majina hayo, moja ya majina yaliyozuiwa huku ni jina la Monkey.
Brazil: Jina lililozuiwa huku ni jina laSaddam Hussein.
Mexico: Wamepiga marufuku mtoto kupewa majina ya Scrotum, Terminator, Burger King,Hitler na Virgin.
Uturuki: Mahakama imezuia mtoto kupewa jina la Osama Bin Laden
Portugal: Wao wamezuia jina la Tom.
Mfano hii ingekuja Bongo, majina gani ungependa yazuiwe wasipewe watoto wetu

0 comments:

-