WATU
wawili wamefariki dunia jijini Dar es Salaam juzi akiwamo Emmanuel
Ndahani (39) mkazi wa Kibamba, aliyegongwa na gari na kufariki dunia
alipokuwa akiweka alama za matawi kuzuia gari zisikanyage maiti.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema Ndahani
aligongwa na gari isiyofahamika kwa kuwa lilikimbia baada ya ajali
hiyo.
Kamanda
Wambura, alisema Yarimunda (36), mkazi wa Kibaha aligongwa na basi hilo
aina ya Scania, juzi, saa 3 usiku maeneo ya Kibamba.
Maiti
zimehifadhiwa Hospitali ya Tumbi Kibaha. Dereva wa basi la Muro,
Boniface Chuwa (36) mkazi wa Kibaha anashikiliwa na polisi.
0 comments:
Post a Comment