Wednesday, December 17

WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA MH HAWA GHASIA.

Serikali imetengua uteuzi wa Wakurugenzi sita
wa Halmashauri, na kuwasimamisha kazi
wengine watano kupisha uchunguzi, kutokana
na kubainika kuchangia kuvurugika kwa
uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika
tarehe 14, mwezi huu.

Akitangaza hatua hiyo kufuatia ripoti
iliyoibua madudu yaliyofanyika katika
uchaguzi huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Mhe. Hawa Ghasia amesema
uamuzi huo pia umeridhiwa na Rais Jakaya
Kikwete.

Mhe. Ghasia amewataja halmashauri ambazo
wakurugenzi hao waliotenguliwa uteuzi wao
kuwa ni za Mkuranga, Kaliuwa, Kasulu,
Serengeti, Sengerema na Bunda,
waliosimamishwa kazi ni wakurugenzi wa
Hanang', Mbulu, Ulanga, Kwimba pamoja na
wa Manispaa ya Sumbawanga.

Waziri Ghasia amesema kuwa Wakurugenzi
wengine watatu wapewa onyo kali, ambao ni
wa Rombo, Busege na Muheza na wengine
watatu wakipewa onyo la kawaida,
wakurugenzi hao ni wa Manispaa Ilala, Hai
na Mvomero.

0 comments:

-