Serikali ya Saudi Arabia imetangaza kuwa, mahujaji wasiopungua 130 wengi
wao kutoka nchi za Kiarabu, wamefariki dunia wakati wa ibada ya Hija
mwaka huu.
Taarifa zinasema kuwa, vifo vya idadi kubwa ya mahujaji vimesababishwa na umri mkubwa na maradhi. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, idadi kubwa ya Mahujaji waliofariki dunia ni kutoka Misri ambapo mahujaji 14 wameripotiwa kufariki dunia.
Nchi nyingine ambazo mahujaji
wao wamefariki dunia ni Iraq, Algeria, Sudan, Morocco, Somalia, Jordan
na Mauritania. Imeelezwa kuwa, mahujaji wengine 213 wamelazwa kwenye
hospitali za Saudi Arabia wakipatiwa matibabu kutokana na maradhi ya
aina mbalimbali.
Hija inahesabiwa kuwa ni moja kati ya nguzo muhimu za dini tukufu ya Kiislamu, na Waislamu wenye uwezo wa kifedha na kiafya kutoka pembe mbalimbali duniani hushiriki kwenye ibada hiyo tukufu katika mji wa Makka.
Mwaka huu, zaidi ya mahujaji milioni mbili
walishiriki kwenye ibada hiyo ya kimaanawi.
0 comments:
Post a Comment