Ni shida! Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, chini
ya Kamanda Mohammed Mpinga, limekuwa mstari wa mbele katika kusimamia
maadili ya askari wake na kuwa mfano wa kuigwa lakini kuna baadhi
wanalichafua, kamchezo kamili kapo hapa.
Polisi wa usalama barabarani wakidendeka.
Habari kamili ikufikie kwamba nyuma ya picha ya askari wawili, mwanamke
na mwanaume wa usalama barabarani (matrafiki) wanaodaiwa kuacha kazi ya
kuongoza magari na kwenda kufanya uchafu kichakani kuna utata mkubwa.
Picha hiyo inamuonesha trafiki mwanamke akiwa amepakatwa mapajani na
trafiki mwanaume aliyekalia kitu kwa chini ili kupata balansi ya kumbeba
mwenzake hukuwawili hao ‘wakifanya yao’ wakiwa na sare za kazi.
TUJIUNGE NA VYANZO
Baada ya picha hiyo kusambaa kwa kasi ya moto wa kifuu kwenye mitandao
mbalimbali ya kijamii usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii na kugeuka
habari ya mjini, watu walikuwa na maoni tofauti huku baadhi wakipiga
simu kwenye chumba chetu cha habari wakitaka kujua ukweli juu ya uwepo
wa tukio hilo.
SIMU YA KWANZA
Simu ya kwanza iliyopigwa ilidai kwamba matrafiki hao ni maarufu katika
Barabara ya Bagamoyo ambapo mara nyingi huongoza magari maeneo ya Tegeta
jijini Dar.
Kamanda Mohammed Mpinga. “Huyo mwanaume ni jamaa mmoja mpole sana anajulikana Tegeta na ana gari aina ya Baloon (Toyota).
“Huyo mwanamke, kwanza ni mke wa mtu lakini yupo bomba (mzuri) kinoma.
Hata madereva daladala wanamjua maana amejaliwa, akitembea lazima
atingishe,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
“Hapo ni maeneo ya Tegeta kwa sababu ukiangalia vizuri kwenye picha hiyo utaona nguzo ya umeme mkubwa wa Zanzibar.”
WHATSAPP
Wakati tukio likiwa ‘hot’, picha hiyo ilitumwa kwenye chumba chetu cha
habari kwa WhatsApp huku ikiwa na maelezo kwamba tukio hilo lilijiri
hivi karibuni mkoani Dodoma bila kufafanua maeneo gani kwa kuwa Dodoma
ni kubwa.
NI KANDA YA ZIWA?
Chanzo kingine kilichozungumza na gazeti hili kilidai kwamba tukio hilo siyo la Dar wala Dodoma ni maeneo ya Kanda ya Ziwa.
“Hilo tukio ni la Kanda ya Ziwa. Itakuwa ni kwenye moja ya Mikoa ya
Kanda ya Ziwa (kati ya Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga, Simiyu na
Geita),” kilidai chanzo hicho. (Ilishathibitishwa kuwa ni Kagera)
IMETENGENEZWA?
Baadhi ya wadau wa jeshi hilo walidai kwamba kuna uwezekano picha hiyo
ni ya kutengeneza (photo shop) kwa kuwa haikujulikana aliyeipiga na
kwamba iliwezekanaje kuwapiga ili hali wakijua ni kinyume na maadili.
“Unajua kinachonifanya nihisi kama imetengenezwa ni namna
walivyojiachia. Kwa vyovyote kuna kitu cha ziada kimefanyika kwenye hiyo
picha,” alisema mmoja wa wachangiaji mtandaoni.
MTAALAM: HAIJATENGENEZWA
Ili kuondoa utata huo wa kutengenezwa au kutokutengenezwa, gazeti hili
lilimwonesha picha hiyo, mtaalam wetu wa kompyuta (IT), Nicolaus Trac
ambaye alithibitisha kuwa siyo ya kutengenezwa.
“Ni vigumu kuwa ni ya kutengenezwa kwa sababu kuu tatu.
“Moja, mandhari ni moja, ingekuwa ya kutengeneza kila mmoja angeonekana tofauti lakini mazingira yanaonesha imepigwa eneo moja.
“Pili, angalia mikono yao ilivyovaana au kuingiliana. Sidhani kama kuna
mtaalam angeweza kuweka mikunjo hiyo ya mikono na vidole bila kukosea
sehemu.
“Tatu, angalia huyo mwanamke alivyomkalia mwanaume, inaonesha kabisa
kumkalia kwake kumesababisha mkunjo katika suruali kwenye paja la mguu
wa kulia,” alifafanua Nicolaus.
PETE YAIBUA MAMBO
Mbali na kukemea tabia hiyo na ukosefu wa maadili hasa kwa mtumishi wa
serikali, wapo baadhi ya watu mitandaoni walikuwa wakimshambulia trafiki
mwanamke kwani picha ilimuonesha akiwa na pete ya ndoa kidoleni.
“Mimi sijui kama huyo trafiki ni mumewe lakini namuona ana pete ya ndoa
maana yake kuna harufu ya mchepuko. “Lakini hata kama ni mumewe, kwa
nini wafanye mambo ya chumbani hadharani tena na sare za kazi? Kama
walikuwa wamezidiwa sana si wangeenda nyumbani?” Alihoji mwanamke mmoja
aliyetumiwa picha hiyo kwenye WhatsApp.
KAMANDA MPINGA ANASEMAJE?
Gazeti hili lilimfowadia Kamanda Mpinga picha hiyo kwa njia ya WhatsApp
ambapo alikiri kuwa nayo na kwamba wanaifanyia kazi kabla ya kuchukua
hatua kali kwa wahusika.
Katika mahojiano ya Kamanda Mpinga hivi karibuni, kamanda huyo
alisisitiza kwamba kikosi chake kinaongoza kwa maadili na kwamba
inapotokea tukio kama hilo hutolewa adhabu kali.
RSS Feed
Twitter
October 10, 2014
Unknown

0 comments:
Post a Comment