Kungu
Masanja ambaye ni mjumbe serikali ya kijiji pia katibu wa Chadema
kijiji cha Chibe katika manispaa ya Shinyanga akiwa ndani ya gari la
polisi muda mfupi baada ya kuonekana na bango kwenye mwenge wa uhuru
kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga-Picha na Kadama Malunde
Kungu Masanja akiwa ndani ya gari la polisi -Picha na Kadama Malunde
Zahanati ya Chibe iliyofunguliwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka huu Rachel Stephen Kassanda-Picha na Kadama Malunde
Hili ndiyo jengo linalodaiwa kujengwa chini ya kiwango,vyanzo vya habari vinasema ndani ya jengo hilo siyo pazuri limejengwa chini ya kiwango-Picha na Kadama Malunde |
Wakazi
wa kijiji cha Chibe kata ya Chibe katika manispaa ya Shinyanga
wamepigwa butwaa baada ya mjumbe wa serikali ya kijiji hicho Kungu
Masanja kukamatwa na askari polisi akiwa ameshikilia bango katika mbio
za mwenge wa uhuru katika kijiji cha Chibe.
Kungu
Masanja ambaye pia ni katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) katika kijiji cha Chibe alikutwa amebeba bango wakati kiongozi
wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka huu Rachel Stephen Kassanda akifungua
zahanati ya kijiji hicho.
Baadhi ya maneno yaliyokuwa yanasomeka katika bango la bwana Kungu Masanja ni ““Kiongozi
wa mbio za mwenge kitaifa,Hivi mapato na matumizi ya zahanati ya kijiji
husomwa wapi?,Hujui jengo la daktari halina kiwango,kama hujui pita
ndani yake”.
Muda
mfupi baada ya kuonekana na bango hilo ghafla askari wa jeshi la polisi
mkoa wa Shinyanga walimkamata na kuondoka naye huku wakazi wa eneo hilo
wakibaki midomo wazi.
Akizungumza
akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi Masanja alidai kuwa
aliyoyaandika yako sahihi na kwamba hajashawishiwa na mtu yeyote ameamua
kuandika ujumbe ili ufanyiwe kazi kama mwananchi mzalendo.
Akizungumza
na malunde1 blog diwani wa kata hiyo Mahona Gwisu Kameja kupitia Chama
Cha Mapinduzi alisema alishangaa kumwona kijana huyo akiwa ndani ya gari
la polisi.
“Binafsi
sikuona bango hilo,wala sikumwona wakati anakamatwa,hilo jengo analodai
liko chini ya kiwango lilijengwa mwaka 2009 kwa nguvu ya
wananchi,serikali na TASAF likigharimu shilingi milioni 52,tangu mwezi
Septemba 2014 linatumiwa na mganga na wauguzi wa zahanati iliyozinduliwa
leo”,alisema diwani huyo.
“Hata
hivyo mimi nashangaa huyu kijana ni mjumbe wa serikali ya kijiji,kama
limejengwa chini ya kiwango basi yeye anapaswa kuwajibika,haiwezekani
mjumbe wa kijiji ajikaange mwenyewe,hapa kuna UCHADEMA maana huyu ni
kiongozi wa Chadema katika kijiji hiki,labda katumwa”,aliongeza diwani
Kameja.
Naye
mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Festo Kang’ombe aliiambia malunde1
blog kuwa jengo hilo limejengwa katika kiwango kinachotakiwa ndiyo
maana linatumika hivi sasa.
Kwa
upande wake kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru 2014 Rachel Stephen
Kassanda alisema jengo lililotengenezewa bango siyo lile la zahanati
waliyoifungua hivyo hawezi kulizungumzia.
Kassanda
alisema mamlaka/majukumu aliyopewa katika mbio za mwenge ni kuzungumzia
miradi iliyoko kwenye ratiba aliyopangiwa hivyo suala hilo wanaohusika
ni halmashauri husika.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alipotafutwa na mwandishi
wa habari hizi kuzungumzia kuhusu kukamatwa kwa kijana huyo alisema yuko
nje ya ofisi,ingawa hata kaimu kamanda wa polisi Longinus Tibishishubwa
alipopigiwa simu zaidi ya mara moja haikupokelewa siku hiyo.
0 comments:
Post a Comment