Tuesday, October 21

Mume aliyejulikana kwa jina moja la Ngosha, mkazi wa Mabibo jijini Dar,
amemfumania rafiki yake aitwaye Jazira akiwa chumbani na mkewe Jack
wakiivunja amri ya sita ya Mwenyezi Mungu.Tukio hilo lilitokea Jumanne
iliyopita saa 12 alfajiri ambapo ilidaiwa kuwa Jack alikuwa chumbani na
mwanaume huyo ambaye ni mpangaji, wenzake wakipeana maraha.
Imedaiwa kuwa, wawili hao walikuwa wakimtegea Ngosha akitoka kwenda
katika shughuli zake, Jazira alikuwa akizama katika chumba cha rafiki
yake na kufanya mchezo wa kikubwa.
Wapangaji wenziye na Jack wamedai kuwa, mke huyo wa mtu ambaye ana miezi
miwili tangu aolewe kutoka mkoani Tabora, amekuwa kero katika nyumba
hiyo kwani amekuwa akipiga kelele za kimahaba nyakati za asubuhi ambapo
watu wengi wanakuwa wakielekea kazini.
“Hata sisi wanawake tunaoishi nyumba hiyo tuna waume zetu tunawalilia
lakini kinachotusikitisha mwenzetu anamlilia Jazira badala ya mumewe
ambaye anakuwa amekwenda kazini,” alisema mmoja wa wapangaji wa nyumba
hiyo.
Imeelezwa kuwa, siku hiyo mlinzi wa msikiti alikwenda kumwamsha Ngosha
kwenda kusogeza gari lake ili watu wapite na alipofika katika chumba
chake, alikuta mlango wa sebuleni ukiwa wazi lakini hakukuwa na mtu, ila
chumbani kwake kulisikika redio ikizungumza kwa sauti kubwa.
Jirani mmoja aliyedai kuchoshwa na tabia hiyo, alimshauri mlinzi huyo
kwenda kusikiliza kwenye dirisha la chumba hicho na waliposikia sauti za
kimahaba wakakubaliana wamtonye mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kanuni,
Mabibo aliyetajwa kwa jina la Asha ambaye alifika na kusikia ‘mchezo’
ukiendelea chumbani
Wakati huohuo, Ngosha akapigiwa simu kuja kushuhudia mchezo huo mchafu wa mkewe alioufanyia ndani ya chumba chake.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema, alipofika Ngosha nyumbani na kutonywa
kilichotokea  alipandwa na hasira na kuangusha varangati kwa rafiki yake
lakini baadaye akatulizwa, akamtaka Jazira amlipe shilingi milioni 1.2
ili amuachie mke moja kwa moja.
JAZIRA ANA LAKI 2
Jazira alisema hakuwa na kiasi hicho isipokuwa anaweza kulipa shilingi
laki mbili tu, jambo lililomfanya Ngosha kuomba msaada wa askari mgambo
na kumpeleka mgoni wake Kituo cha Polisi cha Urafiki kwa ajili ya hatua
zaidi za kisheria.

0 comments:

-