Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ghana, Asamoah Gyan,
amekanusha madai kuwa alimtoa kafara yake ambaye pia alikuwa
mwanamuziki mashuhuri nchini Ghana Castro.
Mwanamuziki huyo aliyekuwa anaiimba nyimbo za mtindo wa Afrobeats,
ambaye jina lake halisi ni Theophilus Tagoe, alitoweka pamoja na rafiki
yake Janet Bandu, mnamo mwezi Julai.
Wawili hao walitoweka wakati walipokuwa wamekwenda likizo na Gyan
ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Sunderland, katika mji wa Ada.
Madai katika vyombo vya habari nchini Ghana yanasema kuwa kutoweka kwa
rafiki ya Gyan kumezua wasiwasi baadhi wakidai kuwa huenda alimtoa
kafara mwanamuziki huyo.
Asamoah Gyan, Akiwa na rafiki yake Castro enzi za uhai wake.
Castro na rafiki yake Bandu, walionekana kwa mara ya mwisho wakielekea baharini na baadaye iliarifiwa kuwa walizama.
Miili ya wawili hao haikuwahi kupatikana na madai yaliendelea
kusambazwa mwezi huu wakati ambapo kakake Gyan, Baffour Gyan alidaiwa
kuwa mmoja wa genge la vijana waliowashambulia wandishi wa habari
waliohoji maswali kuhusu madai hayo.
Hata hivyo baadaye aliachiliwa na polisi waliokuwa wamemkata kwa lengo la kumfungulia mashitaka.
Tetesi hizo zilimfanya Gyan kuitisha mkutano na wandishi wa habari kuzungumzia madai hayo.
Wakili wake Kissi Agbyabeng alitoa taarifa akisema kuwa familia ya Gyan
imeshangazwa sana na madai hayo na iliamua kutosema chochote ili
polisi waendelee na uchunguzi wao.
Taarifa hiyo ilisema: " Tumekuwa kimya huku madai na tetesi zikienezwa
kila upande katika vyombo vya habari. Tumekuwa kimya sio eti kwa sababu
tunaficha ukweli, bali kwa sababu hatuoni umuhimu wa kusema
kilichojiri mjini Ada. Tumekuwa kimya kwa sababu tunataka polisi wafanye
kazi yao bila kuingiliwa.''
Shukran Kwa BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment