Raisi wa
africa ya kusini Jacob Zuma ameshutumiwa kwa kuwa na mfumo wa upendeleo
(Nepotism) baada ya kumteua mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 25
kushikilia cheo kikubwa serikalini.
Thuthukile
Zuma amehamishwa kutoka katika nafasi ya afisa uhusiano wa umma (Public
Liaison officer) na kupandishwa cheo ndani ya miezi miwili akiwekwa
katika nafasi muhimu na yenye nguvu " Mkuu wa wafanyakazi" katika
wizara ya huduma za posta na mawasiliano
Thuthukile ni
mtoto wa mwisho katika watoto wanne wa Zuma, ambae alipokea degree ya
heshima ya Anthropology na kukabidhiwa cheo hicho mwezi wa tano mwaka
huu baadaya baba yake (Raisi Zuma) baada yakuchagua baraza lake la
mawaziri.nafasi hiyo aliyopewa ambayo inasemekana kutokutangazwa kabla, itakuwa ikimuingizia paundi 55,764 karibu randi milioni moja ambayo ni sawa na shilingi 154,631,365.14 kwa mwaka
0 comments:
Post a Comment