Wednesday, August 13


Dkt. David Nabarro, Mratibu wa UM kuhusu ugonjwa wa Ebola.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani na kutangaza kumteua Dkt. David Nabarro kama mratibu mwandamizi wa Umoja wa Mataifa kuhusu ugonjwa wa Ebola.
 "Dkt. Nabarro atawajibika kuhakikisha mfumo wa umoja wa Mataifa unatoa mchango wa dhati katika kuratibu harakati za kimataifa za kudhibiti Ebola."
 Pamoja na uteuzi huo Ban ametaja mambo matatu muhimu kudhibiti Ebola ikiwemo kushughulikia upatikanaji wa rasilimali zinazohitajika ikiwemo fedha na mifumo ya afya, na uratibu wa kimataifa kudhibiti ugonjwa huo, na tatu..
 "Tunapaswa kuondokana na hofu na woga.  Ebola inaweza kudhibitika  kwa rasilimali tulinazo, ufahamu na hatua za mapema. Watu wanaweza kupona ugonjwa huu. Ebola ulidhibitiwa vyema kwingineko na sasa pia tunaweza."
Tayari WHO imeridhia tiba ya majaribio dhidi ya Ebola itumike kutibu wagonjwa wakati huu ambapo zaidi ya watu Elfu Moja wamefariki dunia tangu ugonjwa huo uibuke mwezi Machi mwaka huu hukoGuinea,Liberia,Sierra Leonena sasaNigeria.
Masuala mengine aliyogusia ni mzozo hukoIraqakitaka vikosi vya usalama visiingilie mchakato wa kisiasa na suala la Ukanda waGazaakisema ni matumani yake kuwa kutafikiwa makubaliano ya kudumu ya sitisho la muda la mapigano linalofikia ukomo Jumatano.

0 comments:

-