Mwigizaji wa series ya The Shield Michael Jace amefikishwa mahakamani mjini Los Angeles baada ya kushtakiwa kwa mauaji ya mkewe mwezi uliopita.
Waendesha mashtaka wamesema Jace, alimpiga risasi mara kadhaa mke
wake April Jace aliyekuwa na umri wa miaka 40, nyumbani kwao wakati
watoto wao wadogo wakishuhudia.
Baada ya kufanya tukio hilo Jace alipiga simu polisi kwa mujibu wao na walimkuta nyumbani.
Mwigizaji huyo alicheza kama Detective Julien Lowe kwenye series hiyo ya The Shield.
Maafisa wa kikosi cha zima moto wametoa taarifa ya simu ya dharura
iliyopigwa kwa baba wa April inayobainisha kuwa muigizaji huyo alimpigia
simu kumwambia kwamba amempiga risasi mke wake.
0 comments:
Post a Comment