Mcheza filamu mkongwe wa nchini Marekani Harrison Ford anapatiwa
matibabu hospitalini kutokana na majeraha aliyopata wakati akirekodi
filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Star Wars.
Harrison Ford mwenye umri wa miaka 71 amevunjika kifundo chake cha
mguu baada ya mlango wa eneo la kutengeneza magari kumuangukia wakati
wakirekodi filamu katika studio za Pinewood nchini Marekani.
Mwigizaji huyo wa Hollywood ambaye ameigiza katika filamu ya Star
Wars ambapo sasa anarekodi sehemu ya saba ya mwendelezo wa filamu hiyo
alikimbizwa hospitalini ambapo msemaji wa kampuni ya kutengeneza filamu
amesema wataendelea kurekodi kama kawaida.
Filamu hiyo inaigizwa na wasanii wenginge wakubwa kama Lupita
Nyong’o, John Boyega, Daisy Ridley, Adam Driver, Oscar Isaac, Andy
Serkis, Domhnall Gleeson, na Max von Sydow.
Tukio hilo limetokea wakati wa mwendelezo wa sehemu ya saba ya war Stars ambayo inatarajia kukamilika hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment