Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Gothenberg, Uswizi, wanaume wengi huwapuuza wachumba wao wanapoburudishana faraghani.
Utafiti huo unasema wanaume huongozwa na ubinafsi wanaposhiriki tendo la ndoa na kusahau kwamba wachumba wao wana hisia.
Kulingana na
utafiti huo wa 2009, ingawa wanaume wengi wanaelewa umuhimu wa kuwandaa
wachumba wao kabla ya kuanza burudani,hawajali yanayowapata wenzao
wasipopata shibe la ngoma.
“Suala la
wanaume kutowaridhisha wapenzi wao linatokana na kukosa kuwaandaa vyema.
Mwili wao husisimka haraka wanapopandwa na hamasa ya kushiriki tendo la
ndoa.Wanasahau kwamba mwili wa mwanamke ni tofauti,” yasema sehemu ya
utafiti huo.
Watalaamu wa masuala ya mapenzi wanasema mwanaume mwenye tabia hii huwa hawezi kumfikisha mwanamke kileleni.
Wanasema ni wazi kwamba mwanamke asipoandaliwa vyema, hawezi kufurahia burudani.
“Tabia hii ya
wanaume imefanya watemwe na wachumba wao. Wanawake wanataka mwanaume
anayetambua na kuelewa hisia zao, sio wa kuwatumia kama chombo cha
kutimiza haja zake za kimwili bila kujali wanavyohisi,” asema
mwanasaikolojia Ronald Jameson.
Anasema
mwanaume anayeanza kufanya mapenzi kwa pupa, hawezi kujizuia kufunga bao
baada ya sekunde chache na kumuacha mpenzi wake akitamani burudani.
“Huwa vigumu kwa wanaume wa aina hii kurudia ngoma jambo ambalo wanawake wengi huchukia” asema.
Kujali hisia
“Uhusiano wa
aina hii ambapo wanaume wanajali hisia za wapenzi wao hudumu kwa muda
mrefu, furaha utawala na mapenzi hunoga huku kila mmoja akimwaza
mwenzake kila wakati na kutamani burudani zaidi,” aeleza Jameson.
Anasema mbinu na muda wa kumwandaa mwanamke hutegemea mtu binafsi.
“Kuna
wanawake wanaosisimka wanapoguswa sehemu tofauti za mwili na wengine
hupandwa na hamu ya kufanya mapenzi wanapobusiwa. Wengine wanaingiwa na
hamasa kwa kumtizama mwanaume anayewavutia” asema.
Wataalamu
wanawakosoa baadhi ya wanawake kwa kuchangia misukosuko ya mapenzi hasa
kukosa shibe la burudani kwa kutowaongoza wanaume wao kwa maneno ama kwa
kuweka mikono eneo wanalotaka washikwe ili kuamsha hisia zao za
mapenzi.
“Ni rahisi
kwa mwanamke kufanya mchumba wake ashindwe kusakata ngoma ipasavyo kwa
kutoshiriki kikamilifu katika mechi kitandani” asema.
Wataalamu
wanasema baadhi ya wanawake huwa hawana ujasiri wa kumwongoza mwanaume
kumtomasa sehemu inayoamsha hisia zake za kufanya mapenzi. Jambo hili,
asema Jameson, huwanyima raha ya burudani na kusambaratisha penzi. Hata
hivyo ili kumwandaa mwanamke wa aina hii, watalaamu wanasema mwanaume
anapaswa kutumia ujuzi wa hali ya juu ili kuamsha ashiki zake.
Ili zoezi la
kusakata ngoma lifanikiwe na kufanya uhusiano wa mapenzi huwe thabiti,
mwanamke anatakiwa kuonyesha ushirikiano kwa kutoa miguno na minongono
ya kumchanganya mwanaume.
Kulingana na
utafiti wa chuo kikuu cha Gothenberg, wanawake hawaridhishwi na tabia ya
wapenzi wao kupuuza umuhimu wa kuwaandaa kabla ya kufanya mapenzi.
Watafiti
wanasema wanawake wanachukia wanaume wenye pupa ya kufanya mapenzi. Na
huenda afueni isipatikane kuhusu hali hii huku wanaume wakiwalaumu
wanawake kwa kukosa uwazi katika swala la mapenzi kwa kutowaeleza
wanaume kwamba hawako tayari.
Kukubaliana na utafiti
Wanawake
wengi nchini walikubaliana na utafiti huo wakisema unaeleza jinsi mambo
yalivyo. Wanafananisha hisia za mapenzi za mwanaume na jiko linalotumia
mafuta ya taa linalowaka kwa haraka kisha kuzimika, na mwanamke na jiko
la makaa linalochukua muda kuwaka na halizimiki kwa haraka.
“Mwanamke ni
sawa na jiko la makaa linalohitaji bidii kulichochea liwake, na
likishawaka ni kazi ngumu kweli kulizima,” asema Bi Ruth Wanjiku.
Mwanadada huyu anakiri ushirikiano wa hali ya juu ni muhimu kufanikisha burudani kitandani .
“Ni kweli
wanaume wana haraka ya kufanya mapenzi na humaliza shughuli hata kabla
ya mwanamke kuanza kuwaka. Hata hivyo baadhi ya wanawake wanachangia kwa
kutoshiriki kikamilifu wanaporushana roho,” asema Bi Wanjiku.
Anakubaliana
na watafiti waliofichua kwamba wanawake wanachangia kufanya wanaume
wapungukiwe na nguvu za kufanya mapenzi kwa kutohusika ipasavyo.
“Ni muhimu
kwa wana ndoa au wapenzi kufahamiana vyema ili waweze kusisimuana,”
aeleza Bi Mary Kituyi mkazi wa jiji la Nairobi. Anasema wapo wanaume
wasiowapa wachumba wao nafasi ya kuonyesha ustadi wao wa kurushana roho
“Kuna wanaume
wanaoamini kwamba mwanamke hafai kumfundisha mambo ya mapenzi.
Ukijaribu kumwelekeza unakotaka uguswe au mbinu unayofurahia anaanza
ugomvi,” anasema na kuongeza kwamba uhusiano wa aina hii hauwezi kudumu.
Kulingana na mwanasaikolojia Peter Obonyo wachumba wanaokabiliwa na tatizo hili wanaweza kulisuluhisha bila ya kuachana.
“ Dawa la tatizo hili sio kumwacha mchumba wako, mbali ni kumzungumzia kwa lugha ya mapenzi na sio kwa ukali,” asema.
Anashauri
wanaokabiliwa na tatizo hili wasome vitabu au majarida yanayotoa elimu
juu ya kufanya mapenzi na wataalamu wa mapenzi kwa ushauri.
“ Wakishapata
elimu ya kutosha na kuizingatia, watajitayarisha kisaikolojia na
utashangaa mwanamke anafika kileleni kabla ya mwanaume. Hakuna miujiza
hapa, ni mambo ya kisaikolojia tu,” asema.
Kulingana na mwanasaikolojia huyu wanaowaacha wachumba wao kusaka shibe la mapenzi, hukabiliwa na hatari nyingi.
“Wanaweza
kugeuka kuwa wahamaji wa mapenzi kwa kubadilisha wachumba kila mara. Pia
kuna hatari ya kuathirika kisaikolojia na kukosa utulivu wa kihisia,”
asema.
Maandalizi ya mapema
Kulingana na
wataalamu mawasiliano ni muhimu kati ya wapenzi ili kila mmoja aweze
kumwandaa mwenzake vyema na kwa upendo kabla ya kushiriki tendo la ndoa.
“Maandalizi
huwa kwa njia nyingi.Mazungumzo yenu, usafi wa nguo, mwili na chumba
murua cha kuandalia burudani ni muhimu,” asema na kuongeza kwamba
mwanaume anafaa kuonyesha utulivu na kujali hisia za mpenzi wake.”
Pia mwanamke hafai kuona aibu kumuongoza kipenzi chake ili wafurahi pamoja.
Kulingana na
Bi Wanjiru mwanamme mwenye upendo hufurahi sana ikiwa mpenzi wake
atafunua hisia zake. Anasema kwa kawaida si rahisi wanawake kuelezea
hisia zao kwa maneno na wanaume wanafaa kufahamu ishara za wachumba wao
wakiwa tayari kuteremka katika bahari ya mapenzi.
0 comments:
Post a Comment