Tuesday, May 20

20140519-205430-75270957.jpg
Wakati Manchester United wakifanya uteuzi wa kocha, Barcelona nao waliopoteza taji msimu huu sawa na Man U wamemteua Luis Enrique kuwa kocha wa kikosi chao cha kwanza.
Enrique (44) aliyepewa mkataba wa miaka miwili kuchukua nafasi ya Gerardo Martino ‘Tata’ aliyejiuzulu baada ya kukosa ubingwa, alikuwa kocha wa timu ‘B’ ya Barca tangu 2008 hadi 2011alipokwenda kuwafundisha Celta Vigo mpaka wiki jana.
Barca walishindwa kutetea ubingwa wao kwa kutowafunga Atletico Madrid wikiendi hii kwenye moja ya mechi za mwisho za La Liga na pia walitolewa kwneye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huku wakishuhudia Atletico na Real Madrid wakiingia fainali inayochezwa wikiendi ijayo.

Mkurugenzi wa Soka wa Barcelona, Andoni Zubizarreta anadaiwa kumpendekeza Enrique, aliyepata kufundisha Roma ya Italia kuchukua nafasi ya raia huyo wa Argentina.
Martino (51) alichukua nafasi ya hayati Tito Vilanova aliyekuwa na matatizo ya saratani ya koo, akajiuzulu kabla ya kufariki dunia.
Enrique alitarajiwa kuteuliwa kutokana na ukaribu wake na klabu hiyo na jinsi alivyofanya vyema kwenye timu ya pili alipochukua mikoba ya Pep Guardiola.

0 comments:

-