Amina Ngaluma ‘Japanese’ ni miongoni mwa waimbaji ambao waliipa
umaarufu sana bendi ya African Revolution ‘Tam tam’ kupitia wimbo wa
Mgumba na baadae kujiunga na bendi ya Double M Sound ambapo mpaka
anafariki alikua nchini Thailand akifanya kazi na band ya Jambo
Survivors.
Amina amefariki May 15 2014 saa sita mchana baada ya kuumwa kwa siku nne ambapo mume wake amesema kiongozi wa band yao huko Thailand alimwambia Amina alilazwa hospitali kutokana na maumivu makali ya kichwa.
Ilipofika
Jumapili ndio ilibidi alazwe hospitali baada ya kuzidiwa akapumzishwa
na hivyo akawa hawezi tena kupokea simu ambapo mara ya mwisho kuongea na
mume wake ilikua ni Ijumaa iliyopita.
Amina alikwenda Thailand miezi nane iliyopita baada ya kuongeza
mkataba kuifanyia kazi bendi hiyo ya Watanzania ambayo ina mkataba mrefu
wa kupiga nchini humo.
Msiba upo Kitunda Machimbo kipunguni B nyumbani kwao na kesho ndio
watajua taratibu za kuuleta mwili wa marehemu nchini Tanzania.
R.I.P AMINA NGALUMA JAPANESE
0 comments:
Post a Comment