Kwa
wale wakazi wa magorofani au wanaokwenda na watoto wao kwenye nyumba
hizi zenye urefu kwenda juu inabidi waichukue hii kama tahadhari manake
ni hatari nyingine kwa yeyote.
Madaktari wa watoto wanasema mara nyingi watoto wanapoanguka kwenye
umbali kama huu huwa hawaponi na hata wakibakiwa na uhai bado akili zao
zinakua zimepata majeraha kwa kiasi kikubwa.
Pamoja na hiyo sentensi ya Madaktari, mtoto Musa Dayib
mwenye umri wa
mwaka mmoja ameanguka kutoka kwenye kibaraza cha gorofa ya 11 huko
Minneapolis Marekani lakini amebakiwa na uhai wake japo hali yake sio
nzuri na anapumua kwa msaada wa mashine.
Amevunjika mikono, mgongoni ambapo daktari mwingine wa watoto amesema
Watoto wako flexible na huwa hawavunjiki hawaumii haraka kama watu
wazima.
0 comments:
Post a Comment