Monday, May 5

Screen Shot 2014-05-05 at 5.58.39 PM 
Post hii ni maalum kwa staa wa muziki wa Kenya anaetajwa kuingia kwenye TOP 5 ya Wasanii matajiri wa muziki wa kizazi kipya Afrika Mashariki huku orodha hiyo ikiwa na watu wengine kama Jose Chameleone.
Imefahamika kwamba Jaguar alikataa kuja kwenye tuzo za Kili 2014 alizokua nominated baada ya waandaaji kushindwa kufikia masharti aliyowapa na badala yake akaamua kwenda kuhudhuria harusi ya producer wa DNA aitwae Refigah.

Jaguar alitaka atumiwe ticket ya ndege ya business class, alitaka achukuliwe chumba kwenye hoteli ya nyota tano, apewe ulinzi popote atakapokwenda na vilevile apewe gari zuri la kifahari la kutembelea.
Kwenye sharti jingine Jaguar alitoa option kwa waandaaji na kuwaambia kama wangeshindwa kumpa ticket ya ndege basi walipaswa kuweka mafuta ili aje na ndege yake ndogo anayomiliki.
Chameleone, Wyre, Amani, Ay, Mtangazaji William Tuva, shabiki Daudi wa Kota na friends juzi Dar es salaam.
Chameleone, Wyre, Amani, Ay, Mtangazaji William Tuva, shabiki Daudi wa Kota na Dj wa Chameleone juzi Dar es salaam.
Alipohojiwa na ghafla.co.ke Jaguar alisema asingeweza kuhudhuria tukio ambalo asingepewa heshima aliyoitaka kama ambavyo huwa anaipata anapokwenda kwenye nchi nyingine katika matukio kama haya ndio maana ilikua bora ahudhurie harusi na kuongeza kwamba ‘nitahudhuria iwapo wataanza kuwa-treat vizuri wasanii wa Kenya’
Tuzo za KILI 2014 zilihudhuriwa na mastaa wawili wa Kenya ambao ni Wyre na Amani huku Uganda ikiwakilishwa na Jose Chameleone ambae ndio alitangazwa mshindi kwenye kipengele cha Afrika Mashariki.

0 comments:

-