Meneja Mradi wa Asasi ya
Kijamii ya The Open Society Initiative For Eastern African Tanzania
(OSIEA), Agnes Hanti akiongea wakati wa mafunzo kwa wadau wa Habari
nchini (hawapo pichani) juu ya changamoto zinazowakabili waandishi wa
habari hasa katika haki ya kukuza demokrasia iliyofanyika jijini Dar es
Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi Msaidizi wa OSIEA, Mburu Gitu (Kulia).
Meneja Mradi wa Asasi ya
Kijamii ya The Open Society Initiative For Eastern African Tanzania
(OSIEA), Agnes Hanti akiongea na waandishi wa habari wakati wa
majadiliano.
Waandishi wa Habari na
wadau wa Habari nchini wakijadili juu ya changamoto zinazowakabili
katika haki ya kukuza demokrasia iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa Habari na
wadau wa Habari nchini wakijadili juu ya changamoto zinazowakabili
katika haki ya kukuza demokrasia iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa Habari na
wadau wa Habari nchini wakijadili juu ya changamoto zinazowakabili
katika haki ya kukuza demokrasia iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
—
Asasi isiyo kuwa ya
kiserikali ya OSIEA imesema kazikubwa inahitajika kufanyika ili kulinda
Uhuru wa kujieleza na kujitegemea kwa vyombo vya habari nchini Tanzania.
Wito huo unatokana na kuongezeka kwa vitendo vya kufungia vyombo vya
habari na kuongezeka kwa matukio ya kuwadhuru waandishi wa habari pamoja
na kuingiliwa kwa Uhuru wa wahariri na wanasiasa na wafanyabiashara.
Mwaka jana serikali ili
yafungia magazeti binafsi ya Mwananchi na Mtanzania kwa siku 14 na 90
kwa tuhuma za kuchapisha habari zenye uchochezi ambazo serikali ilidai
zinahatarisha usalama wa taifa na zinatishia uvunjifu wa amani na
umoja.Gazeti jingine la Mwanahalisi liliamriwa kufungwa tangu mwezi
Julai2012 na halijafunguliwa mpaka sasa. Sheria ya magazeti inaipa
serikali mamlaka makubwa ya kukandamiza vyombo vya habari. Hatua zote
hizo zinakwenda kinyume na sheria za nchi na haki za binadamu ambazo
Tanzania imeridhia.
Pamoja ukweli kuwa vyombo
vya habari binafsi vinaongezeka tangia mwaka 1990 lakini Uhuru wa
wahariri wa vyombo hivyo bado una maswali mengi kuhusiana na baadhi ya
vyombo
kutumika kutanga biashara na kuwasaida wengine kisiasa. OSIEA
inaitaka serikali na vyombo vya usalama kuheshimu Uhuru wa kujieleza na
kutoa maoni na kuacha kuwanyanyasa waandishi wa habari. Waandishi wa
habari lazima waweze kuzungumza na kuandika bila ya kuwepo kwa vizuizi
vyovyote. OSIEA pia inaitaka serikali kuwasilisha Bungeni muswaada wa
sheria ya vyombo vya habari ambao utaweka mazingira bora ya Uhuru wa
vyombo vya habari.
Wakati Tanzania ikiwa
katika maandalizi ya kupata katiba mpya, tunahitaji kukumbuka kuwa Uhuru
wa vyombo vya habari na Uhuru wa kujieleza kwa waandishi wa habari ni
kitu cha muhimu kwa ajili ya kusambaza taarifa kwa jamii. Sio tu haki ya
jamii kupokea taarifa bali bila kuwa na Uhuru haitakuwa na maana yoyote
kwa serikali yao. Uwezo wa kupata taarifa utawezesha kukua kwa
demokrasia, kuongeza msisismko wa mijadala ya kitaifa kutoa taarifa
zitakazoongeza uwajibikaji. Uhuru wa kupata habari una mchango mkubwa
katika mchakato wa kupata Katiba mpya.
Licha ya kwamba Tanzania
inakuza uchumi wake wa wakati lakini kusahau Uhuru wa vyombo vya habari
kunaweza kukapunguza ufanisi wa ukuaji wa uchumi. Vyombo vya habari huru
vinaweza kukuza kuimarisha jamii na kuvutia wawekezaji.
0 comments:
Post a Comment