ZOEZI la kuitafuta ndege ya Malaysia iliyopotea yenye namba
MH370, linaweza kugharimu mamilioni ya Dola na kulifanya kuwa zoezi
lenye gharama kubwa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya sekta ya anga.
Zoezi hilo linashirikisha nchi 26 zilizotoa ndege, meli, manowari na satelaiti katika juhudi za kimataifa za kuipata ndege hiyo.Inakadiriwa kuwa tayari zoezi hilo limegharimu Dola Milioni 44 ikiwa ni mwezi mmoja tangu lianze.
Wakati huo huo, kiongozi wa operesheni hiyo, Angus Houston, amesema zoezi la kusaka ishara za chini ya bahari za ndege hiyo huenda likaendelea kwa siku kadhaa kabla mashine ya roboti haijapelekwa kuthibitisha ishara hizo.
0 comments:
Post a Comment