Thursday, April 10

Padre mmoja muitaliano ambaye hakutajwa jina, amekumbwa na mashtaka na fedhea ya kuiba fedha za watawa ili kumpatia mpenzi wake wa kiume kutoka Morocco.

Kiwango cha fedha hizo hakikutajwa ila inakadiriwa kuwa ni maelfu ya Euro ambazo Padre huyo aliaminiwa kuzitunza na watawa hao.

Pesa hizo alizitumia kumhonga mpenzi wake huyo ambaye inaaminika kuwa na mahusiano naye kwa kipindi kirefu sana akishiriki naye mapenzi ya jinsia moja.
 
Imeripotiwa kuwa Padre huyo ameshasimamishwa kuhudumu na Askofu wake.

0 comments:

-