Na Magreth Kinabo, Maelezo-Dodoma
RAIS wa Tanzania, Jakaya Kikwete anatarajiwa kulihutubia Bunge Maalum la Katiba pamoja na kulizinduwa Machi 21, 2014 mjini Dodoma. Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa bunge hilo, Yahya Khamis Hamad wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa ofisi za Bunge mjini Dodoma.
RAIS wa Tanzania, Jakaya Kikwete anatarajiwa kulihutubia Bunge Maalum la Katiba pamoja na kulizinduwa Machi 21, 2014 mjini Dodoma. Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa bunge hilo, Yahya Khamis Hamad wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa ofisi za Bunge mjini Dodoma.
“Kwa mujibu wa kanuni ya 75 (1), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania atalihutubia Bunge Maalum siku ya Ijumaa Machi 21, mwaka 2014
saa 10 jioni, ambapo wageni waalikwa wote watatakiwa kuwa wameingia na
kuketi katika maeneo watakayoelekezwa saa 9:00 alasiri,” alisema Katibu
Hamad.
Alisema ratiba ya shughuli hiyo itaanza na kikao cha Bunge saa 9:10
na baadaye kikao hicho kitaanza saa 9:20 kwa ajili ya kumpokea Rais.
Aliongeza kuwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge, Rais
Kikwete atapokewa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Naibu Katibu
wa Bunge Maalum, ambapo baadaye ataelekea katika jukwaa maalum kwa
ajili ya kupokea salamu za heshima na kukagua Gwaride Maalum ambalo
limeandaliwa na Jeshi la Polisi.
Alisema baada ya shughuli zote kufanyika katika viwanja vya Bunge
utaratibu umewekwa kwa viongozi kuingia Bungeni kwa maandamano maalum.
Viongozi watakaohusika katika maandamano hayo ni Makamu wa kwanza wa
Rais wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar na hatimaye Rais Kikwete ambaye
atafuatana na Mwenyekiti wa bunge hilo.
Katibu huyo aliwataja viongozi wegine walioalikwa kuwa ni viongozi wa
kitaifa na watendaji wakuu kutoka pande zote za Muungano, viongozi wa
kitaifa wastaafu, ambao ni marais wastaafu kutoka pande zote za
muungano, mawaziri wakuu wastaafu, waziri kiongozi mstaafu na maspika
wastaafu.
Viongozi wengine ni mama Maria Nyerere, Mama Shadia Karume na
Mwenyekiti na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Wageni wengine
walioalikwa katika utaratibu huo ni taasisi za dini, taasisi zisizo za
kiserikali, tasnia ya habari, vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa
kudumu, taasisi za elimu, vyama vya watu wenye ulemavu, wafanyakazi,
wafugaji, wavuvi, wakulima na wawakilishi kutoka sekta binafsi.
Kwa mujibu wa ratiba ya shughuli hiyo Rais Kikwete anatarajiwa
kuhutubia bunge hilo kwa muda wa saa moja. Hivyo shughuli hizo
zitakamilika majira ya saa 12:00 jioni.
0 comments:
Post a Comment