
Kumekua na kurasa(accounts) mbalimbali zenye majina ya Mh.Edward Lowasa Waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika mitandao ya kijamii kama vile facebook,twitter,instagram, n.k
zikionesha mmiliki wake ni Mh.Edward Lowassa
Ukweli ni kwamba kurasa hizo hazimilikiwi na Mh.Edward Lowasa mbunge wa Monduli.
Kwa maana hiyo chochote kinachoandikwa au kuchapishwa katika kurasa hizo hazihusiani kwa namna yoyote na Mh.Lowasa
Hata hivyo Mh Lowasa anawashukuru wote wenye kumiliki account hizo bila ruhusa yake,kwani anaamini wamesukumwa kwa mapenzi yao kwake.
Imetolewa na
Ofisi ya Mh.Edward Ngoyai Lowasa
Mbunge wa Jimbo la Monduli.
RSS Feed
Twitter
February 08, 2014
Unknown
0 comments:
Post a Comment