
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kukanusha taarifa
za uvumi zinazosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na vyombo
vya habari kuwa kuna Watanzania wapatao 160 wamenyongwa nchini China kwa
kosa la kusafirisha madawa ya kulevya.
Aidha,
taarifa hiyo ya uvumi imedai kuwa ndugu wa mmoja wa Watanzania hao
ambaye kwa jina anajulikana kama Bw. Rajab Mohamed Ismail Mapusa wamekaa
matanga kuomboleza kifo chake.
Kwa
mujibu wa taarifa rasmi kutoka Serikali ya China, Bw. Mapusa yupo hai
gerezani akitumikia kifungo cha maisha kwa kosa la kuingiza madawa ya
kulevya nchini humo, na hivi karibuni alishiriki kuandaa maonyesho ya
utamaduni wa Kiafrika wakati wa kuadhimisha sherehe za Mwaka Mpya wa
China.
Wizara
inapenda kuwakumbusha Wanahabari kuandika taarifa ambazo ni sahihi
zisizopotosha Umma kwa kuzingatia weledi, maadili na ukweli kutoka
mamlaka zote husika.
Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam
10 Februari, 2014
RSS Feed
Twitter
February 10, 2014
Unknown
0 comments:
Post a Comment