Tarehe kama ya leo mwaka 1958 yaani ( 6 February 1958) – Miaka 62
iliyopita, timu ya soka Manchester united ikiwa na kikosi chenye vijana
wastani wa miaka 24 kinachoaminika kuwa imara kuwahi tokea katika
historia ya klabu hiyo chini ya kocha Matt busby na kupewa jina la
“Busby Babes” kilikuwa kinasafiri kutoka
Yugoslavia ambapo walitoka
kucheza dhidi ya Red star Belgrade ya nchini humo katika kombe la ulaya
yaani ” European Cup”
Ilipofika Ujerumani katika uwanja wa Munich Riem Airport ilibidi
watue ili ndege iongezewe mafuta, baada ya hapo katika jaribio la tatu
kupaa ndege hiyo ikagonga baadhi ya majengo ikaanguka na kuanza kuwaka
moto!
Hii ni video inayoonesha tukio lilivyotokea.
Ndani ya msafara huo kulikuwa na jumla ya watu 44, kati yao kulikuwa
na wachezaji, maofisa wa timu, waandishi wa habari na mashabiki ambapo
watu 20 hapo hapo walipoteza maisha huku wengine wakikimbizwa katika
hospitali ya Recht der Isar ya jijini Munich ambapo dakika chache watu 3
walikufa na kufanya idadi ya waliokufa kufikia 23 na 21 walinusurika
huku kocha mkuu Matt Busby alinusurika akiwa mahututi na kapteni ambaye
hadi leo huwa anaonekana katika mechi za Manchester United akiwa kama
mmoja wa wakurugenzi wa bodi ya klabu hiyo Bobby chalton akinusurika
salmini!
Katika watu 23 waliokufa kwenye ajali hiyo, wachezaji 8 walikufa hapo
hapo na maofisa 3 wa timu, wengine walikuwa mashabiki na waandishi.
bonyeza hapa chini kucheki video ya ajali hiyo
RSS Feed
Twitter
February 06, 2014
Unknown
0 comments:
Post a Comment