Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) leo February 21 limetangaza
matokeo ya mtihani wa kidato cha Nne kwa mwaka 2013 na kuainisha kuwepo
kwa wanafunzi wengi waliopata daraja Sifuri ambao ni asilimia 42.91 ya
watahiniwa wote.
Matokeo hayo pia yameonyesha wasichana wakiwa wamefaulu kwa asilimia
56.73 na wavulana wamefaulu kwa asilimia 59.58 huku nafasi za juu za
ufaulu zikishikiliwa na wasichana na shule binafsi huku shule nyingi
zilizoshika nafasi za mwisho kumi ni za Serikali.
Matokeo hayo yametangazwa na Dk. Charles Msonde ambaye ni Kaimu
Mtendaji wa Nectana kubainisha kuwepo kwa wanafunzi 10 waliofutiwa
matokeo yao baada ya kuandika matusi ambapo matokeo ya wanafunzi 31,518
yamezuiliwa kutokana na madai ya ada.
Wanafunzi walioruhusiwa kurudia mitihani mwaka 2014 ni 23 ambao
hawakufanya baadhi ya masomo na wanafunzi 24 waliopata matatizo ya
kiafya.
0 comments:
Post a Comment