Saturday, December 14

photo 1
Tumezoea kusikia na kuwaona wasanii wa muziki wa Nigeria wakija Tanzania kufanya show kitu ambacho huwa sio stori hata kwao, yani wao kuja kufanya show sio stori kutokana na ukubwa wa muziki wao kwenye nchi za Afrika, Tanzania tunawajua wengi kutoka kwao kama P Square, D’Banj, Davido, Wizkid, Iyanya, J Martins na wengine ila nchi yao bado haijaujua muziki wa bongofleva.

Basi hii lazima iwe stori kubwa kwetu Tanzania manake Vanessa Mdee anakua msanii wa kwanza wa bongofleva kualikwa kwenda kufanya show kwenye stage moja na wakali wao Lagos Nigeria ambao ni pamoja na P Square, D’Banj, Wizkid, Davido, 2Face na wengine ambapo staa wa dunia Wyclef Jean ni miongoni mwa watakaohost show hii.
Hii stori inazidi kunoga baada ya V Money kusema hawa jamaa ndio waliamua kumualika hivyo wakawasiliana na Meneja wake ambae ni Abby wa 102.5 Choice FM Dar es salaam.
v moneyHii ni good news kwa bongofleva manake kwa kipindi kirefu Wasanii wa Tanzania wamekua wakihangaika kupenyeza kwenye soko la Nigeria ndio maana hata TV yao kubwa ya burudani (Sound City) ilipoanza kupiga video za Ay na Diamond, imekua stori kubwa kwa sababu Nigeria ni taifa lililogumu kuupa nafasi muziki wa nchi nyingine ukiachia mbali muziki wa Marekani.
Kama wamevutiwa na V mpaka kumpa time kwenye stage mbele ya maelfu ya mashabiki ambao hujitokeza kila mwaka kwenye tamasha hili, hii sio habari ndogo.
V Money ambae anamiliki mawimbi kwa hits kama Closer, Come over na me & you aliyoshirikishwa na Ommy Dimpoz, ameiambia millardayo.com na AyoTV kwamba amepewa dakika 5 tu za kuimba kwenye hiyo stage ya show ambayo ni kama ‘Fiesta’ yao Jumapili ya Dec 15 2013.
photo 2
Tunaweza kuifanya hii stori kuwa kubwa kwa kutweet sana hii habari na pia kwa kumtweet bila kuchoka @VanessaMdee na hashtag ya #VmoneyLagos kumpa moyo na support kwa ujumla kuanzia sasa mpaka Jumapili yenyewe siku ya show, pia tunaweza kuhusisha tweet zetu na kumention majina ya mastaa wa Nigeria watakaofanya nae show ili wajue kabisa kuna kichwa kutoka Tanzania kipo nao.

0 comments:

-