Tuesday, September 17

                
ASSALAAM Alaykum/Bwana Asifiwe. Wiki iliyopita nilipokea maswali mengi kutoka kwa wasomaji wangu wa safu hii, wakiniuliza kuhusu hina, asmini, kilua na mrangiragi. Sikuweza kujibu kwa mtu mmoja mmoja lakini leo kupitia hapa, natoa majibu yote.ali ya
yote, nianze kwa kuwatupia lawama makungwi wanaowafunda wanandoa na kushindwa kuwafundisha vitu hivi, unatakiwa kumueleza mwari wako maana ya udi, asmini, kilua na hina. Ajue vitu hivi vina maana gani kwa mwanamke mwenye ndoa yake.
Somo asiyefikisha ujumbe kwa mwari wake huwa namwita feki, kwani toka nianze kuandika nimekuwa nikiulizwa mambo mengi ambayo naamini kuwa kama mtu kapitia kwa kungwi lazima atakuwa anayafahamu

MAFUNZO SASA 
Leo nitoe mafunzo ya mambo haya kwa ufasaha kabisa. Shosti wewe ambaye hujui ndiyo ukae kitako unisome kwani utapata faida na utaidumisha ndoa yako.
Unachukua maua ya asmini, majani ya mrangirangi, kilua na pompiyo. Kwa pamoja unaviweka kweye kitambaa ambacho unakifunga na uzi. Fundo hilo ndilo linaitwa kuba la asmini.
Shoga wewe si wa kileo? Basi fundo hilo liweke kwenye cheni yako halafu vaa shigoni au kiunoni.
Ukishavaa, kazi inakuwa kwa mwanaume, kwani yeye ndiye mwenye ruhusa ya kulikata hilo kuba la asmini.

ATALIKATAJE? ENDELEA KUNIFUATILIA
Mwanaume aliyekamilika, aliyefundwa akafundika anajua jinsi ya kulikata hilo kuba. Halikatwi kwa mkasi wala kiwembe, linakatwa kwa meno bibi.
Unaweza kuvaa lililochanganywa na vitu vyote shingoni kisha la asmini pekee ukavaa kiunoni, utaniambia huko utakachokutana nacho. Kuba lina stali yake ya kukatwa, ni ufundi tu wa mumeo.

UDI NA MISK
Wanawake wengine wameumbwa na maumbile yenye jasho lisilovumilika kwa mume. Utakuta mtu anamtesa mumewe kwa kulala amegeukia ukutani mpaka asubuhi, akiamka anaanza kutangaza eti mume wake anamnyima haki yake.
Shoga jichunguze sana, hakikisha mumeo anakuwa nawe kwa furaha zote, siyo yupo nawe kutimiza tu wajibu.
Paka misk kwenye kiungo, inaondoa harufu mbaya yote. Ni pafyum ya asili, isiyokuwa na tatizo lolote mwilini.
Udi mwanamke ni lazima kila siku asubuhi na jioni. Ujifukize ili kukifanya chumba kinukie na wewe unukie, kwa nini mumeo ahamie kwa jirani kwa sababu ya harufu nzuri wakati zinauzwa madukani? Jiulize mwanamama na uchukue hatua.
Epuka ubize wa maisha kwani utajikuta unampoteza mwanaume ambaye ni muhimu sana katika maisha yako. Kila siku nakwambia kuwa mambo yanayokuweka bize unaweza kuyapata lakini mume utampata wapi?
Tokomeza kansa ya ndoa, mpende mwanaume wako, mpe haki yake ya kila siku. Epuka kulala na nguo, shuka tu inatosha. Oga vizuri na unapotaka kulala hakikisha unafuata yale niliyokufundisha, zingatia mlo sahihi, mwisho kumbuka kusema asante kwa mumeo.
Wiki ijayo tukutane kwa mada nyingine.

0 comments:

-