Saturday, September 7

Mshike mshike wa maandalizi ya bonanza la 8 la vyombo vya habari maarufu kama media bonanza mkoa wa Arusha umepamba moto baada ya viongozi wa TASWA mkoa wa Arusha kutangaza zawadi kwa WASHINDI

                   
                                           
                  Katikati ni katibu wa Taswa  Arusha Bwana  Mussa Juma akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari na kulia kwake ni Mwenyekiti Msaidizi Taswa Bw Andrea Ngobole huku kushoto akiwa mhamasishaji wa michezo kutoka TBL.

Akizungumza jana na waandishi wa habari mkoani arusha katibu wa TASWA mkoa wa arusha ndugu Musa Juma alizitaja zawadi hizo kama ifuatavyo:
mshindi wa kwanza kwenye mpira wa miguu atapata kombe la dhamani ya shilingi laki 2 na fedha taslimu shilingi laki mbili na nusu.Mshindi wa pili atazawadiwa fedha taslimu shilingi laki moja.
Aliendelea kueleza kuwa sambamba na mpira wa miguu pia kutakuwa na mashindano mengine kama netball,kuvuta kamba na kukimbiza kuku huku pia wakihaidi zawadi nono kwa washindi.
  Sambamba na hilo pia kutakuwa na zawadi kwa mtu mmojammoja kwenye mchezaji bora  wa mpira wa miguu na mpira wa mikono ambapo kila mshindi atapata fedha taslimu shilingi 50000.
Makamu Mwenyekiti wa Taswa Andrea Ngobole akizungumza jambo na Mjumbe wa Taswa Bwana Shija
Mashindano hayo yatakayofanyika katika viwanja vya general tyre njiro,tarehe 08 mwezi wa 9 2013 yatapambwa pia na burudani kutoka club ya taikwondo na bendi ya vita mult band                             
                       
Mhamasishaji wa michezo kutoka TBL Bwana Deodatus Katambi akizungumza jambo na waandishi wa habari

  Mashindano hayo ya 8 yanayoandaliwa na  MCunity na TASWA Arusha yatatimua vumbi kuanzia majira ya saa 3 asubuhi huku tukikumbuka kuwa bingwa mtetezi ni AJTC chuop cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha.
                     
 kiongozi wa band ya vita mult plus akizungumzia maandalizi ya band yao kwenye tamasha hilo
Mashindano hayo yanahisaniwa na TANAPA,TBL,MEGATRADE LTD,AICC COCA COLA NA PEPSI,DARE FOR MORE....

0 comments:

-