Sunday, July 28

Carzola avunja ukimya kufuatia tetesi za kuhamia Atletico Madrid

Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla amesisitiza kwamba hana mpango wa kuondoka klabuni kwake pamoja na tetesi zinazomuhusishwa kuondoka majira ya kiangazi. 
 
Muhispania huyo amefurahia kuanza mechi za pre-session Arsenal na kulikuwa na tetesi kwamba atakwenda Atletico Madrid.
 
Ingawa Cazorla amekiri kwamba siku moja atarudi La Liga, amesema hana haraka kuondoka Emirates kwa sasa.

"Mengi yamesemwa kuhusu Atletiko Madrid, Lakini najisikia vizuri kuishi London," Cazorla alikiambia chombo cha habari vya ESPN hivi............ "Bado nina mkataba na Arsenal na nitaanza mazoezi Jumatatu.”

"Tutaona nitakaporudi kwenye La Liga – kwa sasa ni vigumu."

Cazorla alijiunga na Arsenal akitokea Malaga majira ya joto ya msimu uliopita.

Arsena yamng'ang'ania Luis Suarez

Arsenal imeamua kuwa king’ang’anizi kwa Luis Suarez, pamoja na Liverpool kukataa ofa zake 2, The Gunners wanajiandaa kupeleka ofa nyingine ya tatu.
The Gunners wako tayari kuhamisha mbingu na nchi kuhakikisha wanamsajili straika mwenye ubora ili kuimarisha nafasi ya mshambuliaji, na straika huyo si mwingine ni Luis Suarez hii ni baada ya kumkosa nyota wa Real Madrid Gonzalo Higuain aliyetimkia Napoli ya Italia mapema wiki iliyopita.
Liverpool wamekataa ofa mbili za Arsenal na wamesisitiza kwamba hawako tayari kumuuza nyota huyo kwa mahasimu wao wowote wa Ligi ya Uingereza.
 
Nyota huyo mwenye Umri wa Miaka 26 alifanya mazungumzo Meneja Brendan Rodgers na Mtendaji mkuu Ian Ayre Alhamisi. Lakini klabu imekataa kuweka bayana kwamba mkutano huo uliendaje jambo ambalo The Gunners walitafsiri kama ushindi wa kumnasa nyota huyo.
 
Arsenal imetoa dau la pauni milioni 40 kwa ajili ya nyota huyo wa zamani wa Ajax wakitumaini kwamba ingeishawishi Liverpool kumwachilia nyota huyo lakini ikawa tofauti.
Wekundu hao wa Anfield wamebaki ving’ang’anizi kwamba pauni milioni 40 kwa mujibu wa mkataba wake haimruhusu Suarez kufanya mazungumzo na klabu nyingine lakini inampa haki ya kujua tu kwamba kuna klabu imeleta ofa kwa ajili yake na klabu tu ndiyo yenye maamuzi ya mwisho.
 
Arsenal haijawahi kutumia zaidi ya pauni milioni 15 kwa mchezaji yeyote katika Historia yao ya hivi karibuni na sasa wanalazimika kutoa angalau pauni milioni 15 zaidi ya ofa yao ya mwisho ili kupata fursa ya kufanya mazungumzo.
Jose Mourinho kumtoa kwa mkopo Bertrand Traoré
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amevutiwa na shughuli ya  Bertrand Traoré, na ana matumaini kwamba kiungo huyo wa Burkina Faso atapewa kibali cha kufanya kazi baadaye mwaka huu.
Mourinho amesema anatambua kwamba kibali cha kufanya kazi kinaweza kisitolewe kwa Traoré, ambaye anatimiza umri wa miaka 18 mwezi Septemba, kwa maana hiyo Chelsea italazimika kumtafutia klabu atakayocheza kwa mkopo kwa muda.
“Traoré anapenda kubaki,” Kocha huyo raia wa Ureno alikiambia chanzo cha Telegraph. “Hizi ni Taratibu za Uingereza na tunapaswa kuzikubali. Tunahitaji kusubiri hadi atakapotimiza umri wa miaka 18 ndiyo ataruhusiwa kubaki Uingereza. Na kama haiwezekani, tutamruhusu kwenda kwa mkopo kokote.”
Traoré alifunga goli kwenye ushindi wa 4-1 dhidi ya Malaysia XI.
"Ni kijana mdogo, lakini najua atakuwa na nafasi nzuri Chelsea hapo mbeleni," Alieleza beki wa Chelsea Gary Cahill.
Man United Iko tayari kutoa kitita cha pauni milioni 80 kumrudisha Cristiano Ronaldo Trafford.
Imeripotiwa kwamba Man United imefufua nia yake ya kumsajili nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo. Wababe hao wa Old Trafford wakitafuta namna zote kuborasha kikosi wakati wakijitahidi kumshawishi Wayne Rooney kubaki
Chanzo cha The Manchester Evening News kimedai kwamba Man United itajitahidi kumbakisha Rooney, pia baada ya kupata ugumu kumleta Fabregas Old Trafford wamehamishia nguvu zao kwa Ronaldo kwa mara nyingine.
Chanzo hicho kimesema Manchester United haitasita kutoa kiasi cha pauni milioni 80 Real Madrid inayotaka kwasababu ndiyo bei waliyomuuza nyota huyo kwa wababe hao wa Ligi ya Hispania miaka minne iliyopita na bei hiyo na nzuri tu ukizingatia kwamba mchezaji huyo amekuwa bora zaidi baada ya kucheza Hispania kwa muda sasa.
Ronaldo amefunga mabao magoli 201 katika mechi 199 alizocheza Real Madrid Na kwa kipindi chote hicho amenyakua taji moja tu la La Liga na moja la Copa del Rey.
Gareth Bale kulazimisha kwenda Real Madrid
Gareth Bale amemwambia mwenyekiti wa Tottenham Hotspur Daniel Levy kwamba anataka kwenda Real Madrid, kwa mujibu wa gazeti la Hispania Marca. Habari zinasema kwamba nyota huyo wa Wales amemtaka mwenyekiti wake kuheshimu makubaliano waliyofanya mwaka jana.
Kwa mujibu wa Habari toka Hispania, makubaliano yalikuwa: 
Klabu itamruhusu Gareth Bale kwenda Santiago Bernabeu endapo hawatafuzu ligi ya mabingwa Ulaya.
"Uliniahidi kwamba endapo hatutafuzu ligi ya Mabingwa na Ofa nzuri itakuja utaisikiliza. Vema, sasa ofa imekuja na ninataka kwenda Real Madrid. Kwahiyo timiza ahadi yako sasa na ukubali kufanya mazungumzo." Bale alikaririwa akimwambia Levy.
Fowadi huyo amekuwa akitajwa kwa mara tisa sasa kuhusishwa na uhamisho kwenda Real Madrid wakati huo Florentino Perez akikiri hadharani kwamba anataka kumsajili nyota huyo.
Mabingwa wa Ligi ya Uingereza Manchester United nao pia wamehusishwa na nyota huyo, na bosi mpya David Moyes akikarirwa mara kadhaa akisema kwamba anao uwezo wa kushindana na Real Madrid. 
Hata hivyo Bale ameeleza azma yake ya kutaka kucheza Ligi ya Mabingwa jambo ambalo Tottenham Hotspurs haiwezi kufanya msimu huu jambo ambalo litawakata maini Old Trafford chanzo cha Marca kilimkariri Bale akisema anataka kwenda Real Madrid.
"Sivutiwi na Manchester United wala klabu nyingine yoyote ile. Nataka kuichezea Real Madrid tu".
Mkataba wa Bale Hotspur unaisha 2016. Meneja Andre Villas-Boas amethibitisha mazungumzo kwa ajili ya kuongeza mkataba.

0 comments:

-