Hili ni sakata la
kikongwe
mmoja anayedaiwa kumiliki idadi kubwa ya madanguro katika uwanja wake na
kuwapangisha makahaba katika eneo maarufu kwa jina la Kijiji cha
Makahaba.
Mwandishi wetu alipokea ujumbe mfupi ulioelezea ufuska
unaofanywa na mabinti ambao hupewa eneo na kujenga vibanda kisha kujiuza
kwa bei chee katika kijiji hicho maeneo ya Kigamboni jijini Dar.
Bada ya simu hiyo, uchunguzi wetu ulibaini kwamba, eneo hilo linalofanyiwa
ufuska huo linamilikiwa na kikongwe aliyejitambulisha kwa jina la mzee
Matutu akidaiwa kuendesha maisha kwa biashara hiyo ya madanguro.
Baada ya kujiridhisha na uchunguzi kuwa ni kweli jambo hilo
linafanyika eneo hilo,waandishi walivamia eneo la tukio wakiwa na mjumbe wa mtaa huo
aliyefahamika kwa jina la Abbas na kujionea madanguro yaliyojengwa kwa
mstari ambapo milango yake iliachwa wazi huku ndani wakionekana mabinti
wakiwa wamejilaza kihasarahasara wakiwatega wateja wanaopita katika mtaa
huo.
Madanguro hayo ambayo kwa hesabu ni takriban kumi na nane,
yamejengwa kwa aina yake ambapo mengi kati ya hayo yana ukubwa wa
kutosha kuingia kitanda kidogo pekee.
Baada
ya kujionea hayo, kikosi kazi sambamba na mjumbe huyo kilimtafuta mzee
Matutu na kufanikiwa kuzungumza naye kuhusu madanguro hayo na namna
anavyoyaendesha ambapo alikiri kuwa yeye ni mmiliki wa eneo hilo na huwa
anapokea shilingi 30,000 kwa mwezi kwa kila mwanamke na fedha hiyo
ndiyo inayomsaidia kuendesha maisha.
Kwa
upande wake mjumbe wa mtaa huo, Kassim alisema kuwa serikali ya mtaa
imejitahidi kwa kadiri ilivyoweza kuwaondoa mabinti hao lakini wamekuwa
wakirudi kila mara.
Alipoulizwa hatua waliyoichukua kwa mmiliki wa
madanguro hayo ambaye ni mzee Matutu, kiongozi huyo alibakia kusikitika
asijue hatua gani ya kumchukulia mzee huyo ambaye hata wakimpeleka
kwenye vyombo vya sheria anahisi itakuwa ni uonevu kwa kuwa hana msaada
mwingine wa kifedha zaidi ya fedha kutoka kwa mabinti hao.
0 comments:
Post a Comment